Mwenyekiti wa Kamati ya Maandali ya Tamasha la kuombea Amani
na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Alex Msama akifafanua jambo Dar es Salaam,
mwishoni mwa wiki, wakati akimtangaza Rais Jakaya Kikwete kuwa mgeni rasmi
katika tamasha hilo, litakalofanyika Oktoba 4 kwenye
uwanja wa Taifa. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo,
Hamisi Pembe. (Picha na Loveness Bernard)
NA
MWANDISHI WETU
RAIS wa Jamnuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha maalumu la kuombea amani Uchaguzi Mkuu
uliopangwa kufanyika Oktoba 25.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo, Alex Msama alisema ni faraja
kubwa kwao kuona Rais anakubali mwaliko wao wa kuwa mgeni rasmi.
“Tumefurahi sana kuona
Rais wa nchi anakubali kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la kuombea amani
Uchaguzi Mkuu kwa manufaa ya taifa letu, sisi tukiwa waratibu wa tukio hili
tumefarijika mno,” alisema Msama.
Alisema tukio hilo litakalowaleta pamoja
viongozi wa kada zote wakiwamo wale wa madhehebu na dini mbalimbali bila
ubaguzi, litasindikizwa na burudabi ya nyimbo za injili kutoka kwa waimbaji wa
ndani na nje ya nchi.
Msama alisema Kamati ya
maandalizi iliamua kumuomba Rais Kikwete sio tu kwa kutambua nafasi yake katika
taifa, pia moyo wake wa kuhimiza amani wakati wote wa utawala wake ikiwemo
kushiriki matamsha ya injili.
Alisema, mbali ya
kuwaongoza Watanzania kuombea taifa lao lipite salama katika uchaguzi mkuu, pia
wadau wa muziki wa injili watalitumia tukio hilo kumuga na kumshukuru kwa mchango wake
katika kukuza muziki wa injili.
Akifafanua nafasi ya Rais
Kikwete kukuza muziki huo, Msama alisema katika harakati zake za kuratibu matukio
ya muziki wa injili, kiongozi huyo amewahi kuwa mgeni rasmi katika tamasha la
Pasaka mwaka 2011.
Msama alisema kitendo cha
Kikwete kutokuwa mbaguzi wa dini, ndio maana Kamati ya kuratibu Tamasha la kuombea
Amani Uchaguzi Mkuu imempa heshima kutokana na kuwa kielelezo cha amani na
mshikamano.
Alisema ujumbe mahususi
katika Tamasha hilo ni kwamba, suala la amani na utulivu, ni jukumu la kila
mmoja kwa nafasi yake kwani thamani ya tunu ya amani haiwezi kuonekana kwa
wepesi hadi pale inapotoweka.
Msama alisema Kamati yake
imejitwisha jukumu hilo
la kuhimiza amani katika uchaguzi mkuu kutokana na kuwepo kwa viashiria vya
uvunjivu wa hiyo amani kutokana ushindani mkali uliopo katika uchaguzi wa
safari hii.
Ushindani mkali katika
uchaguzi huo umetuama kati ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Edward Lowassa anayeungwa mkono na vyama vinne ninavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) na Dk. John Magufuli wa CCM.
Msama alisema, baada ya
uzinduzi kufanyika Uwanja wa Taifa siku hiyo ambapo kiingilio kitakuwa sh 5000;
3000 kwa wakubwa na sh 1,000 kwa watoto, tamasha hilo litaelekea katika mikoa 10 kuhamasisha
amani.
Miongoni mwa waimbaji wa
kigeni waliothibitisha kushiriki na nchi zao kwenye mabano ni Solly Mahlangu na
Sipho Makhabane (Afrika Kusini), Ephraem Sekereti (Zambia), Anastazia Mukabwa
na Solomon Mukubwa Kenya.
0 comments:
Post a Comment