Nafasi Ya Matangazo

September 13, 2015

4
Msanii akilimiki jukwaa.
Meneja biashara wa kituo hicho cha Radio Bi ANGELA MAINA alisema kuwa maana halisi ya kufanya zoezi hilo ni kuwapa vijana nafasi ili kukuza vipaji vyao hasa katika tasnia ya music ili miaka ijayo watanzania waone matunda ya kazi hiyo haswa kwa washiriki wa zoezi hilo.
Aidha meneja masoko na mahusiano wa RADIO 5 Bi SARAH LAZARO alisema kuwa pamoja na lengo kuu la mchakato huo ni kuvumbua na kunyanyua vipaji lakini pia ni nafasi kwa wadau wa biashara na mashirika binafsi haswa yanayojihusisha na maswala ya kijamii kuanza sasa kushirikiana na radio 5 ili kukuza biashara zao na kushiriki katika kuendeleza jamii.
3
DJ Haazu akiwajibika.
Radio 5 imekuwa na michakato mbalimbali ili kusaidia vijana katika secta tofauti tofauti zinazohusu maisha yao ya kiuchumi huku ikiwa inawaunga mkono vijana wenye shughuli mbalimbali ambao hufika radioni hapo kuomba saport ikiwa ni pamoja na vijana wa sarakasi,ujasiriamali na fani nyingine. Mchakato ambao sasa unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao umezinduliwa Jijini Dar es salaam na kupewa jina la RADIO 5 KAMATA KIPAJI katika viwanja vya TP sinza darajani ilishughudiwa vijana wengi wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuibuka na zawadi mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.
2
WAfanyakazi wa RADIO 5 wakishangilia wakati Wasanii mbalimbali ambao ni vijana wenye vipaji wakati wakionesha vipaji vyao jukwaaji (kulia), Mtangazaji wa Redio 5 Mwangaza Jumanne (katikati), Meneja masoko na mawasiliano Sarah Keiya na kushoto ni Meneja Vipindi, Mathew Philip.
Katika zoezi hilo vijana walitakiwa kutuma nyimbo zao radioni ikiwa ni pamoja na kujiandikisha majina yao ili siku waandaaji hao watakapofika katika mtaa waliopo basi waweze kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao,na kupatikana washindi ambapo mchakato huo utapita katika maeneo yote ya jiji la Dar es salaam na mwisho kuwapata washindi wanne ambao ndio watakaoibuka na zawadi kabambe. Lengo kuu la mchakato huo ni kuwasaka vijana ambao wanavipaji na wapo mtaani kutokana na sababu mbalimbali ambazo wameshindwa kuonyesha vipaji hivyo ambapo RADIO 5 wameamua kupita katika mitaa hiyo kuhakikisha kuwa vijana hao wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji walivyo navyo kwa watanzania.
16
Umati wa mashabiki waliojitokeza kushuhudia wasanii wenye vipaji jukaani.
DSC_0166
Mtalamu wa kiduku.
  14 
  DSC_0180
Kulia ni DJ Haazu, pamoja na wasanii. PICHA ZAIDI >>>FK MATUKIO
Posted by MROKI On Sunday, September 13, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo