NIZIARA ya kwanza ya
kihistoria kwa kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis kuzuri
Marekani tangu achaguliwe kushika wadhifa huo.
Papa Francis mwenye umri wa
miaka 78, ameingia nchini marekani jana baada ya kumaliza ziara yake ya siku nne
nchini Cuba ambako atakaa kwa siku tano atakuwa katika miji ya Washington DC,
New York na Philadephia ambako pia maadhimisho ya Umoja wa
Mataifa ambapo zaidi ya viongozi wa juu Duniani 100 watakuwa katika mji huo wa
New York.
Lakini tofauti na viongozi
wengine mbalimbali wanaowasili nchini humo na kupewa heshima kubwa na ya
mapokezi huku wakitumia magari ya kifahari, Papa Francis ameweka rekodi na kuwa
kiongozi pekee aliyeamua kutumia gari dogo aina ya Fiat 500 rangi nyeusi.
Akiwasili katika uwanja wa
Ndege wa kijeshi wa Andrews uliopo mjini Washington, Papa Francis alipokelewa
na mwenyeji wake Rais Baraka Obama wa Marekani kisha kumtambulisha kwa mkewe na
familia yake, Makamu wa Rais Joe Biden kisha viongozi wengine wa juu wa taifa
hilo na kuondoka uwanjani hapo wakiwa katika magari tofauti.
Papa Francis ambaye kwa kawaida ni mnyenyekevu, aliondoka kwa kutumia gari hilo dogo Fiat 500
huku likisindikizwa na kulindwa vilivyo na magari ya usalama na Rais Baraka
Obama akiondoka katika gari lake aina ya Beast ambalo kamwe haliwezi kutetereka
na bomu la aina yeyote kwa jinsi lililovyotengenezwa.
Papa akiondoka akiwa ndani ya kari dogo aina ya Fiat 500
Alipowasili uwanjani hapo huku akilakiwa na Rais Barack Obama wa Marekani, Familia yake na viongozi wengine wa juu wa Marekani.
Rais Barack Obama akisalimiana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis.
Papa Francis akiwa mwenye furaha na mwenyeji wake
Akisalimiana na Familia ya Rais Barack Obama.
Papa akiondoka
Gari lililo mbeba Papa Francis likiondoka uwanjani hapo.
Msafara wa Papa mitaa ya D.C.
0 comments:
Post a Comment