Rais wa Shirikisho la Riadha
Tanzania (RT), Anthony Mtaka akipokea msaada wa wa vifaa vya michezo kutoka kwa
mwakilishi wa kampuni ya Nike, Rebet Jones mjini Beijing China. Mtaka yupo
nchini China akiwakisha RT katika mkutano mkuu wa IAAF na kupiga kura kumchagua
kiongozi mpya.
**********
Wanariadha hao Fabian Joseph, Alphonce
Felix na Ezekiel Jaffery ambao watashindani katika marathon wakati Ismail Juma
atashindana katika mbio za mita 10,000. Mashindano hayo yatafanyika kwenye
uwanja wa Taifa wa Beijing maarufu kwa jina la Kiota cha Ndege.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania
(RT), Anthony Mtaka alisema kuwa wanatarajia kupata medali kupitia wanariadha
hao kutokana na maandalizi
waliyoyafanya.
Mtaka ambaye yupo China alisema kuwa wanariadha hao
wapo katika hali nzuri na morali yao ipo juu tayari kuiwakilisha vyema nchi
yao.
“Wanariadha wetu wapo katika hali nzuri na
lengo lao kubwa ni kushinda katika mbio hizo, wanaoshiriki marathon wataingia
uwanjani alfajiri wakati Ismail ataingia uwanjani jioni kuwania medali pia,”
alisema Mtaka.
Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Hai, alisema kuwa Rais mpya
wa Shirikisho la Riadha Duniani, Lord Sebastian Coe ameahidi kuisaidia Tanzania
katika kuboresha mchezo wa riadha.
“Nimezungumza naye na ameahidi kutupa sapoti kubwa na kurejesha
heshima ya mchezo huo kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma, nimefarijika sana,”
alisema.
Katika hatua nyingine Mtaka alisema kuwa RT limepokea msaada wa
vifaa vya michezo vya timu ya shirikisho hilo kutoka kwa kampuni ya Nike vifaa hivyo watatumia wanariadha wetu
waliopo Beijing.
Alisema kampuni hiyo imetoa msaada huo kufuatia maombi
yaliowasilishwa RT mapema mwaka huu ambapo pia kampuni hiyo imeahidi kuuanga
mkono mchezo huo kwa kuendelea kutoa msiaada ya vifaa vya michezo katika
mashindano yajayo ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment