Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Rehema Mkamba akikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na LAPF kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo.
Mwalimu
mkuu wa shule ya Sekondari Dodoma, Marco Masala akizungumza wakati
wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa
na LAPF.
Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bi. Rehema Mkamba akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi
vilivyotolewa na LAPF
Baadhi ya Wanafunzi wa Dodoma Sekondari waliohudhuria hafla hiyo.
Mwanafunzi wa kidato cha sita Sabina John akitoa neon la shukurani kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma.
Mfuko
wa Pensheni wa LAPF leo hii unakabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi
vyenye thamani ya shillingi millioni mbili kwa uongozi wa Shule ya
Sekondari Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa uzio,baada ya kupokea ombi la
kuchangia ujenzi huo.
LAPF
inaamini kuwa msaada huu utasaidia kuchangia gharama na hatimaye
kufikia lengo la kukamilisha ujenzi huo na kuhakikisha usalama wa
wanafunzi. Msaada huu utawanufaisha si tu Wanafunzi na Walimu
wa Shule ya Sekondari Dodoma bali pia wadau wengine mbalimbali ambao
wamekuwa wakitumia viwanja vya Shule hii kwa michezo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na watumishi wa LAPF.
LAPF
imekua ikitoa misaada mbalimbali ya kijamii hasa kwa wadau muhimu kama
Shule za Msingi na Sekondari,Vituo vya Afya, Vituo vya Watoto yatima ,
kuchangia michezo nk.
LAPF ni Mfuko wa Pensheni ambao pamoja
na majukumu mengine, jukumu lake kuu ni kutoa mafao ya Pensheni kwa
wanachama wake. Mafao yanayotolewa na LAPF ni pamoja na;
· Pensheni ya Uzeeni.
· Pensheni ya Ulemavu.
· Pensheni ya Urithi.
· Fao la Uzazi.
· Mikopo ya kujikimu.
· Mikopo ya elimu .
· Mikopo ya nyumba.
· Mikopo kwa wanachama wa kupitia Saccos.
· Mikopo kwa Wastaafu.na
· Msaada wa mazishi.
Kwa
sasa Mfuko wa pensheni wa LAPF unaandikisha wanachama kutoka sekta zote
kama vile Waalimu, Watumishi wa Afya, Wajasiliamali nk.
MAISHA POPOTE NA LAPF
0 comments:
Post a Comment