Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) Kanda ya Kaskazini,Annette Mahimbo Matindi.
Wananchi
wanaofika kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji(Taso)Nane nane Njiro
jijini Arusha wametakiwa kufika kwenye banda la TCRA kujifunza mambo
mbalimbali yanayohusiana na Mamlaka hiyo muhimu kwa wananchi na uchumi
kwa ujumla.
Meneja wa Mamlaka
ya Mawasiliano(TCRA) Kanda ya Kaskazini,Annette Mahimbo Matindi amesema
kuna umuhimu mkubwa wananchi kufahamu utendaji kazi wa taasisi hiyo
badala ya kuilalamikia bila kujua mipaka na wajibu wake.
Amesema wakulima na
wafugaji ili kunufaika katika shughuli zao hawana budi kutumia kwa
usahihi huduma za mawasilino ili kukuza biashara zao.
"Nitumie fursa hii
kuwataka wananchi wote kutumia kwa usahihi huduma za mawasiliano badala
ya matumizi yasiyofaa na ambayo wakati mwingine watajikuta kwenye mikono
ya vyombo vya dola,"amesema Annette
Amesema wakulima na wafugaji ni sehemu muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania hivyo mawasiliano ni nyenzo muhimu kwao.
0 comments:
Post a Comment