Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John
Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini katika mkutano wa hadhara
wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa saba saba.Magufuli amesema
akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataendeleza juhudi zake za kujenga
barabara kwa kiwango cha lami,amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa
Ujenzi katika kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.
Amesema tangu
kupewa kuwa waziri wa ujenzi ameweza kujenga barabara zaidi kilomita 7000
nchi nzima,ambapo ilipelekea kuongeza kuongeza pato la mfuko wa barabara kutoka
bilioni 73,3 hadi kufikia bilini 866 kwa mwaka huu hivyo ameahidi akiwa rais
atajenga zaidi barabara za lami.
Dkt MAGUFULI
ambae anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mikoa ya nyanda za juu kusini
, amelalamikia udanganyifu wa baadhi ya mitandao ya kijamii na baadhi ya
vyombo vya habari kuripoti kuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika
hospitali ya mkoa wa mbeya wakati sio kweli.
Aidha pia Magufuli amewaomba wananchi waweke imani
kubwa kwake kwa kumpa kura nyingi zitakazomwezesha kuwa
raisi wa awamu ya tano,na kIsha alipe fadhira hizo kwa kutatua kero
zinazowakabili hasa wananchi wenye kipato cha chini.SOMA ZAIDI FK MATUKIO
0 comments:
Post a Comment