Bondia nyota nchini wa
ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka atapigana na bondia wa Uingereza, Martin
Murray katika pambano maalum lisilo la ubingwa la uzito wa Super Middle.
Pambano hilo limepangwa
kufanyika mjini Manchester Septemba 19 na maandalizi yake yamekwisha kamilika.
Meneja mpya wa bondai huyo,
Juma Ndambile alisema kuwa Cheka ataondoka hapa nchini Septemba 15 kwenda
Uingereza kwa ajili ya pambano hilo la raundi 10.
Ndambile ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security alisema kuwa ameamua kuingia
mkataba wa mwaka mmoja na Cheka ili kuresha heshima yake katika mchezo huo na
pambano la Uingereza ni la mtoano kwa ajili ya kuwania ubingwa wa Dunia.
Alisema kuwa Cheka
anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya dola za
Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata la
ubingwa. Alisema kuwa endapo atashinda pambano hilo, atasaini mkataba mwengine
za zaidi ya dola 25,000 ili kupigana pambano la tatu.
“Lengo ni kumfanya bondia
bora ili hata akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini
yangu pia nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato,
nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.
Alisema kuwa Cheka amekuwa
na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea kutokana na mambo
ya ‘kidunia’ na yeye ameakua kumkwamua kabisa.
Cheka alisema kuwa
amefurahi sana kupata meneja mpya ambaye tayari amemtafutia pambano nje ya nchi
na sasa imebakia kwake ni kufanya kazi tu. “Ndambile amenilipia kambi ya zaidi
ya Sh milioni 2 hapa jijini, nakaa mimi na kocha wangu, naahidi
kufanya vyema kwenye pambano hilo,” alisema Cheka.
0 comments:
Post a Comment