Kikosi cha Yanga ambacho leo kimekubali kichapo cha bao 2-1 na Gor-Mahia ya Kenya.
Wababe wa Yanga timu ya Gor-Mahia
Yanga ndio walikuwa wakanzwa kupata bao katika dakika 4 baada ya mlinzi wa nyuma wa Gormahia kujifunga lakini dakika 12 baadae wakasawazisha kupitia Harun Shakav.
Yanga walicheza wakiwa pungufu baada ya mshambuliaji wake Mzimbabwe, Donald Ngoma kulambwa kadi mbili za njano zilizozaa nyekundu na akatolewa nje katika dakika ya 24.
Yanga itajilaumu baada ya nahodha wake kukosa penati katika dakika 17 kufutia adhabu baada ya mchezajio wa Gor Mahia kuunawa mpira eneo la hatari.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam timu ya APR ya Rwanda imeanza vyema safari ya kulitaka kombe hilo linalodhaminiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Shandy ya Sudan. goli lilofungwa na kiungo Bizimana Djihad, dakika ya 64.
Aidha katika uwanja wa Karume palikuwa na mchezo mwingine uliowakutanisha KMKM kutoka Visiwani Zanzibar na Telecom ya Dijbout.
0 comments:
Post a Comment