Afisa Mtendaji
Mkuu wa EAG Group Imani kajula Akiwa Pamoja na Rais Wa Simba Sport Club Evans
Aveva wakati wa Uzinduzi wa Simba Day.
**********
Dhima ya Simba Sports Club ya
kuendeleza mabadiliko ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika
kipindi cha miezi mitatu sasa, mmekuwa mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta
mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa, kujali wanachama, wapenzi
wake na kukuza vyanzo vya mapato.Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi Simba
Week 2015 Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Kila mwaka timu yetu ya Simba
imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku maalum kwa ajili ya kufurahi,
kuwatambulisha rasmi wachezaji, jezi za timu na kujiandaa kwa msimu mpya, siku
hii imekuwa maarufu kama Simba Day. Tangu ianzishwe imekua ikiboreka siku hadi
siku, mwaka huu tumeona ni muhimu kuiboresha zaidi na hususani kuangalia
mchango wa timu yetu kwa jamii inayoizunguka’’.
Aliongeza kusema ‘’Hivyo basi
mwaka huu tunaanzisha Simba Week ambayo lengo lake kuu ni kuwa wiki ya Simba
Sports Club kufanya kazi za jamii, kukuza vipaji vya soka vya vijana,
kutembelea wadau wa maendeleo na pia shughuli nyingine zenye tija kwa timu yetu
na jamii kwa ujumla. Wiki hii itahitimishwa siku ya Simba Day ambapo mambo mengi
mazuri yatafanyika. Tofauti na miaka mingine, tutatengeneza program ambayo
itawashirikisha wana Simba Nchi nzima.
Tunategemea kuwa na siku za
kujitolea kwa jamii, wapenzi wote wa Simba Nchi nzima watajitokeza kufanya
shughuli za kijamii kwenye maeneo yao. Simba inaamini kwa dhati tukiunganisha
Nguvu zetu tunaweza kuleta madabiliko makubwa sana Nchini kwetu’’.
Pia Rais huyo wa simba
Alisema, Napenda kuwataarifu rasmi kuwa siku ya Simba Day, Simba Sports Club
itacheza mechi na AFC Leopards ya Kenya kwenye mechi hii wachezaji wetu wapya
wataonekana rasmi baada ya maandalizi ya kutosha, kabla ya mechi hii kutakuwa
na mechi kali ya utangulizi kati ya Viongozi wa Simba na Bongo movie ambao
watachanganyika na Bongo Flava, mechi hii nina uhakika itakuwa burudani tosha.
Jambo jema na jipya ni kuwa Kiingilio cha siku hii ni BURE!. BURE kwa wanachama
wa Simba ambao watakuwa na kadi mpya za Simba hivyo nawaomba wanachama
wachangamkie fursa hii kwa kuchukua kadi mpya!. Simba itaendelea kujali
wanachama wake mara zote!
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa EAG Group amabo ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara
wa Simba, Imani Kajula alisema ‘’ Siku ya Simba Day jezi mpya za Simba zitaanza
kuuzwa rasmi, napenda kutumia jukwaa hili kutahadharisha wauza jezi feki kuwa
mkono wa dora utawafikia.
Kwa wale wanaotaka kuwa
mawakala au wauzaji wa jezi za Simba milango iko wazi wawasiliane nasi kwa
anuani zilizopo kwenye tovuti ya klabu www.simbasports.co.tz au kufika kwenye
klabu ya Simba. Pia wapenzi wanaotaka kuwa wanachama wanaweza kujiunga kupitia
tovuti ya klabu na mawakala kwani kwa kuwa mwanachama wa Simba Sports Club
mwanachama anapata faida nyingi ikiwemo bima ya maisha hadi 250,000 ikiwa
mwanachama atafiwa na mwenza, mtoto au yeye mwenyewe akifariki’’
0 comments:
Post a Comment