Napenda kutoa taarifa fupi kuhusu
tukio lililotokea tarehe 11/07/2015 majira ya saa 10:00 hrs huko katika Hoteli
ya St. Gasper hapa mjini Dodoma, kuwa wananchi walitoa taarifa majira ya saa
10:00 hrs kwamba kuna mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia amekamatwa na wananchi
akiwa na fedha nyingi na kuna vurugu kubwa. Baada ya kupata taarifa hizo, Jeshi
la Polisi Mkoani hapa lilifika eneo la tukio ili kuona kama taarifa hizo ni za
kweli.
Askari walithibitisha kuwa ni kweli
walimkuta mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia ambaye alijulikana kwa jina la AMIT KEVALRAMANI
mwenye umri wa miaka 31, Mhindi, Mfanyabiashara, Mkazi wa Dar es Salaam akiwa na fedha kiasi cha Tshs. 722,500,000/=
ambacho alipohojiwa alisema kuwa tarehe 10/07/2015 alifika Dodoma kwa ajili ya
ununuzi wa mazao ya nafaka. Alipofika Dodoma tarehe 10/07/2015 majira ya
asubuhi alifikia katika Hoteli ya St. Gasper na tarehe 11/07/2015 aliamua
kurudisha fedha benki kutokana na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka na
wenye viashiria vya vurugu.
Akiwa katika harakati ya kurejesha
fedha hizo benki, ndipo kundi la watu waliokuwa katika eneo la Hoteli ya St.
GASPER walimtilia mashaka na kumzuia asiondoke na ndipo taarifa zilitolewa
polisi. Mashaka ya watu hao yalitokana na vuguvugu za kisiasa/mchakato wa
uchaguzi kati ya makundi mbalimbali kuwa kuna watu wanahonga wajumbe. Taarifa
za aina hiyo ambazo hata Jeshi la Polisi lilikuwa limepokea bila uthibitisho.
Katika tukio hili na uchunguzi
tulioufanya tumebaini kuwa hakuna kosa la jinai lililothibitika licha ya
kukutwa na kiasi hicho cha fedha, tuhuma za rushwa ambazo ndiyo zilikuwa msingi
wa ukamataji wa mtu huyo hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona akizigawa
fedha hizo wala hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo.
Aidha imethibitika fedha hizo ni
mali yake halali na kwa kuwa hakuna ushahidi mwingine uliyo thibitisha
vinginevyo amerejeshewa fedha zake.
Imetolewa
na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
0 comments:
Post a Comment