Viongozi wa juu wa Umoja wa vyama vya Upinzania nchini Tanzania ujuliakanao kama UKAWA, umetangaza rasmi kumkaribisha Kada wa Chama cha Mapinduzi na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli anaemaliza muda wake, Edward Lowassa kujiunga na moja ya vyama vinne vinavyounda Umoja huo wa Katiba Nje ya Bunge. Viongozi hao wa Ukawa wamesema wapo tayari kumpa nafasi endapo atajiunga nao apeperushe Bendera ya vyama hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
MWENYEKITI mwenza wa Vuguvugu la Umoja
wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Profesa Ibrahim Harouna Lipumba,
(katikati), ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, akizungumza kwenye mkutano
na waandishi wa habari makao makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam
leo Jumatatu Julai 27, 2015. UKAWA imetangaza rasmi kumpokea kwa mikono
miwili Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, kujiunga na vuguvugu
hilo.
Aidha habari za ndani ya UKAWA zinaarifu kuwa viongozi wa juu wa Vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, NLD na CHADEMA, wamekubaliana kumsimamisha Mh. Edwarxd Lowassa, ambaye awali alikuwa mwana chama wa Chama Cha Mapinduzi, CCM kusimama kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia umoja huo kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Kesho Jumanne Julai 28, 2015 jijini Dar es Salaam, anatarajiwa Edward Lowassa kuzingumzia suala hilo.

0 comments:
Post a Comment