Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, (kulia), akikabidhi fomu za wadhamini za kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi, (CCM), kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015, kwa Naibnu Katibu Mkuu wa chama hicho, (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi, kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama, mjini Dodoma leo Julai 1, 2015. Mh. Lowassa amepata wadhamini mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na jumla ya wana CCM 874,297 wamemdhamini kuwania kiti hicho.
Mh. Lowassa akilakiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi, kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo Julai 1, 2015
Mh. Lowassa akiwa na Mkewe Mama Regina Lowassa, akiziweka sawa fomu hizo
Mh. Lowassa, akitoa taarifa fupi mbele ya waandishi wa habari baada ya kurejesha fomu
Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Geita, Msukuma, akizungumza baada ya Mh. Lowassa kutoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari
Mh. Lowassa, (katikati), akiwa na mkewe Mama Regina, na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, akisoma taarifa hiyo
Mh. Lowassa akiwapungia wana CCM waliofurika ukumbi wa ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma Julai 1, 2015, baada ya kurejesha fomu
Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Hamisi Mngeja, akizungumza
Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
Mh. Lowassa, akiteta jambo na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru mjini Dodoma
Mh. Lowassa, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, mjini Dodoma Julai 1, 2015
Mh. Lowassa na wenyeviti wa CCM wa mikoa
Mh. Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa
Mh. Lowassa, akipunga mkono wananchi waliofika kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wakati akiondoka na gari lake.
*************
*************
WAZIRI Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli mkoani
Arusha, Mh. Edward Lowassa, amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania
kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu wa 2015.
Mh. Lowassa ambaye
alikuwa amesindikizwa na Wenyeviti wa CCM wa mikoa 12 kutoka bara na
visiwani, aliwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma majira ya
saa 8;30 mchana Julai 1, 2015, na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(Tanzania Bara), Rajabu Luhavi.
Baada ya kukabidhi fomu hizo, Mh.
Lowassa, alikutana na waandishi wa habari na kusoma taarifa yake fupi,
ambapo alionya wale wote wanaoeneza habari potofu kuwa yeye ni mla
rusha, watoe ushahidi, wapi amekula rushwa, na ni kiasi gani, za nani
na wapi, Awataka Watanzania kupuuza habari hizo na kwani yeye ni
muadilifu na hana shaka na hilo.
Alisema, yeye ana fedha kiasi gani za
kuwapa Wana CCM 874,297, waliojitokeza kumdhamini.
"Maneno hayo sasa basi, natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi huo
autoe hadharani vinginevyo waache kueneza uvumi na uongo" Alisema Mh.
Lowassa.
Alisema yeye anachukia umasikini, na
kwamba endapo chama kitamteua na hatimaye Watanzania kumchagua kuwa Rais
wa awamu ya Tano, atahakikisha anatimiza dhamira yake ya kuwaondolea
Watanzania umasikini.
Mh. Lowassa, ambaye alisindikizwa na Vigogo wa
chama hicho akiwemo, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, na Mzee Pankrans
Ndejembi wakiwemo wenyeviti wa CCM 12 kutoka Tanzania Bara na Visiwani,
amehitimisha zoezi hilo baada ya kuzunguka mikoa 31 ya Tanzania Bara na
Visiwani, na mara zote amekuwa akipata idadi kubwa ya wana CCM na
wananchi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM mahala alikopita, ikiwa ni
pamoja na wengine kujipanga barabarani na kumpungia mikono
0 comments:
Post a Comment