Nafasi Ya Matangazo

July 17, 2015

Mwanamuziki wa muziki wa dansi aliyepata kushika chati za juu katika utunzi na uimbaji katika bendi mbalimbali nchini za muziki wa Dansi, Ramadhani Masanja 'Banza Stone' amefariki dunia hii leo m,chana nyumbani kwao Sinza Kijiweni Dar es Salaam. Anaandika Father Kidevu.

Kwa Mujibu wa Mmoja wa wanafamilia ya Marehemu, Banza anataraji kuzikwa kesho saa 10 jioni katika makaburi ya Sinza.

Aidha Mwanafamilia huyo amesema Mwili wa marehemu kabla ya mazishi utaswaliwa Lion uliopo Sinza Dar es Salaam. 

Banza Stone atakubwa na wengi hasa kutiokana na nyimbo zake nyingi ambazo ziliweza kuwabadili watanzania na hulka ya kuwapenda wanamuziki wa nje hasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Banza stone alijizolea umaarufu mkubwa wakati alipojiunga na kuanzisha bendi ya Afrika Stars 'Twanga Pepeta' iliyo tamba na kiionjo cha Kisima cha Burudani Eeeebaba!! 

Katika sanaa hiyo ya muziki Banza alianza harakati za muziki miaka ya 1990 wakati huo akisoma elimu ya dini ya Kiislamu katika madrasaBanza aliwahi kufanyakazi na bendi ya Twanga Pepeta, African Stars, TOT, Bambino na Extra Bongo .

Mionongoni mwa nyimbo ambazo banza atakumbukwa nazo ni Mtu Pesa, Sisi ndo Sisi, Mtaji wa Masikini, Utanikumbuka, na ile inayotumiwa sana na wapenzi wa Simba, Angurumapo Simba Mcheza Nani.

Nyimbo hizo aliimba na wasanii mbalimbali aliokuwa akifanya nao kazi kama Ali Choki, Luiza Mbutu, Super Ngedere na wehngineo wengi. 

JENERALI BANZA STONE AMETOKA WAPI!! 
Ramadhani Masanja 'Jenerali Banza Stone" Alizaliwa Oktoba 10, 1972 katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam 20/10/1972 akiwa ni mtoto wa Mwisho katika familia ya Mzee Ally Masanja iliyokuwa na watoto nane.

Akiwa anaishi Lumumba, Banza alipata elimu yake ya msingi Shule ya Mnazi mmoja kabla ya kuingia kwenye sanaa ya muziki.

Alikuwa akisoma pia elimu ya dini ambayo aliishika sana na hata akiwa madrasa alikuwa akiimba sana kaswida na akaamua kuanza mziki kwa kushiriki katika vikundi vya mtaani.

Alianza muziki katika kikundi cha disco kilichoitwa Octimas na baadae alihamia kundi cha DBR  na mwaka 89 akaanzisha kikundi cha disco cha Home boys akiwa na Elvis Danger (mpwa wake), Ashura Mponda na Ras Dee.

Mwaka 92 akaenda kusoma muziki chuo cha Korea Culture alipomaliza akapiga deiwaka Twiga band kabla ya kuanza rasni muziki na Afri Swez. 

Kipaji kilipozidi kupanda akaenda African Stars Twanga Pepeta, TOT, akarudi Twanga na baadae akaanzisha bendi yake ya Bambino Sound hii ikiwa ni mwanzoni mwa 2000.

Banza hakudumu na bendi yake akahamia Chipolopolo, akarudi tena kuifufua Bambino lakini haikusimama akarejea Twanga na kukaa kidogo kabla ya kwenda kuungana na swahiba wake Ali Choki aliyeanzisha Bendi ya  Extra Bongo  na mpaka anafariki dunia bendi yake ya mwisho kuifanyia kazi ni BM.

Akapata deiwaka na Bendi ya Rungwe iliyokuwa na maonesho yake mjini Mbeya na show ya mwisho ni mwezi Februari mwaka huu alipougua na kurejeshwa kwa  ndege jijini Dar akaendelea kuumwa mpaka anafariki leo.

Banza Stone ameacha mtoto mmoja aitwae Haji Ramadhani Masanja.
Posted by MROKI On Friday, July 17, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo