Mwenyekiti
wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon
Anastaz Mpanju ambaye pia alikuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Mpya amejitokeza hii leo sambamba na wana CCM wengine katika safari ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Kawe Wilaya ya Kinondoni.
Akizungumza na Father Kidevu Blog, katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Mpanju amesema huu ni wakati muafa kwake kuwatumiakia wana Kawe.
Mpanju ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, amesema wanakawe wananafasi sasa ya kuandika historia ya aina yake si tu kumchagua mtu mlemavu bali kumchagua, kijana na mchapakazi mwenye uwezo wa kutetea na kuwasilisha hoja za kuleta maslahi kwa kawe na taifa.
“Huu
ni wakati wa wananchi wa Kawe kuandika historia ya aina yake, sit u kwa
kumchagua mtu mwenye ulemavu kuwaongoza bali kijana mwenye uwezo wa kutetea
hoja na maslahi yua wananchi na taifa kwa ujumla,”alisema Mpanju.
Mpanju
amekuwa ni mwananchi wa 16 kujitokeza kugombea jimbo la Kawe na ni mwana CCM wa
39 kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya
chama hicho.
Mwenyekiti
wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon
Mpanju akizungumza na wanahabari . Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman
Sheshe.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman
Sheshe akimsaidia kutia saini ya dole gumba Mpanji.
Mwenyekiti
wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon
Mpanju akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman
Sheshe, kwaajili ya kuomba ridhaa ya
wana CCM Kinondoni kumteua kugombea Ubunge Jimbo la Uchaguzi la Kawe katika uchaguzi
mkuu Oktoba mwaka huu.
Nae
Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athumani Sheshe (pichani), amempongeza Mpanju kwa
uamuzi wake huo na kusema kuwa anatekeleza moja ya kanuzi na sheria za Chama
kuwa watu wote ni sawa na walemavu wanahaki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa
vipongozi.
“Mimi
nitoe wito kwa watu wote wenye ulemavu nchini ambao wanasifa na vigezo
vinavyotakikana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini wajitokeze na
kufanya hivyo na watatendewa sawa sawa na wengine bila ubaguzi au
unyanyapaa,”alisema Sheshe.
0 comments:
Post a Comment