Nafasi Ya Matangazo

July 22, 2015



Meneja uhusiano wa Airtel, bwana Jackson Mmbando akiongea na mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Geita na Mtwara  walipatikana akichukua taarifa za mshindi (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada  Airtel bwana Fabian Felician.(kati) droo hii imechezwa leo katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam,
 ***************
 Airtel yatangaza washindi wa kwanza wa droo ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" Jumanne 21 Julai 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imechezesha droo ya kwanza ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" nakutangaza washindi wawili wa kwanza wa wiki waliojishindia kila mmoja  pesa taslimu.

Akiongea kuhusu droo ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema"Promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" itawawezesha watanzania kujinga na kushiriki bure na kupata nafasi ya kujishindia shilingi milioni moja kila wiki na mwisho wa promosheni
kujishindia milioni mbili. Lakini mteja anawea kuamua kujiongeza na kushiriki kwa tozo ya shilingi 300 kwa siku na kupata nafasi ya kujishindia zawadi nono zaidi ikiwa ni pesa taslimu shilingi milion 3
kila wiki na mwisho wa promosheni mteja ataweza kujindia milioni 50.

Akitangaza washindi Mmbando alisema" Leo tumechezesha droo ya wiki ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa promosheni ya  "Jiongeze na Mshiko" wiki iliyopita. Ninayo furaha kutangaza washindi ambao ni pamoja na Plasikus Gabriel Balimasu (25) Mlinzi na mkazi wa wa Mkoa wa Geita yeye amejishindi shilingi milioni 3 , na  mshindi wa pili ni Rashidi Hassan Mshabaha (27) mfanya biashara ndogondogo na mkazi wa mkoa wa Mtwara yeye amejishindi shilingi milioni 1

"Tunaamini ushindi huu utawawezesha wateja wetu kupata fedha za kuendesha shughuli zao za uchumi na kuboresha maisha yao, hilo ndilo lenge letu kama Airtel kupitia kampaini yetu ya"its now" inayolenga
kuwawezesha na kuwainua watanzania kuzifikia ndoto zao.  Natoa wito kwa watanzania kujiunga na kushiriki bure kwa kutuma ujumbe wenye neon BURE kwenda namba 15470 na kupata nafasi ya kushindia kupitia droo zetu za kila wiki." aliongeza Mmbando.
Posted by MROKI On Wednesday, July 22, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo