Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo mmoja
utakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
wenyeji timu ya Azam FC watawakaribisha Mabingwa wapya wa ligi hiyo
msimu huu timu ya Young Africans.
Mechi
hiyo no. 141 itachezeshwa na mwamuzi wa kati Jacob Adongo kutoka Mara,
akisaidiwa na washika vibendera Frednand Chacha (Mwanza), Hellen Mduma
(Dsm), huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hussein Kalindo (Dsm) na Kamisaa
wa mchezo huo ni Damian Mabena kutoka Tanga.
Katika
mchezo huo timu ya Young Africans itakabidhiwa Kombe lake la Ubingwa wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2014/2015, na mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr
Fennela Mkangara.
Mchezo
huo wa kesho unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 kamili jioni, kwa saa
za Afrika Mashariki na kati ili kutoa fursa kwa wadau, wapenzi na
mashabiki wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kushudia mchezo huo pamoja
na shamrashamra za kukabidhiwa kikombe.
Young
Africans watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu
na mgeni rasmi, huku wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi
ya Vodacom wakimkabidhi zawadi mchezaji bora wa mwezi Aprili Mrisho
Ngasa na fedha taslimu sh. millioni moja.
0 comments:
Post a Comment