KIPENGA cha watangaza nia wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) ni kama kimeshapulizwa, hii ni kutokana na kasi ya hao wanaotaka kuwania
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama tawala kuanza
harakati na kutoa ratiba zao kuutangazia
umma nia yao.
Wapo ambao wamesha tangaza hadharani nia yao hiyo
ya kukiomba chama kuwapa ridhaa ya kuwaomngoza watanzania na pia kukiongoza
chama hicho kikongwe Tanzania.
Jumamosi hii taifa lita shuhudia kada wa Chama
hicho na Mbunge wa Monduli aliyepata kuwa
Waziri Mkuu, Edward Lowassa atatangaza nia yake ya kuomvba ridhaa ya
chama chake kumpa nafasi ya kuwania Urais katika uchaguzi mjkuu utako fanyika
Oktoba mwaka huu.
Lowassa atafuatiwa na Kada mwingine na Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Charles Makongoro Nyerere nae anataraji
kutangaza nia yake ya kuwaomba wana CCM wenzake kumpa nafasui ya kuwania urais
akiwa Butiama.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe nae wakati wowote atafanya hivyo huko kijijini kwake
Chiponda Rondo, Mkoni Lindi. Idadi ya wana CCM waliotaka kuwania nafasi hiyo
mwaka huu ni kubwa na huenda kulinganisha na miaka ya nyuma.
Pia vyama vya upinzani navyo watu wengi wanaweza
jitokeza kuwania nafasi hiyo, kupitia vyao na kupitia umoja wao waliouanzisha
wakati wa Bunge la Katiba kuwa watasimamisha Mgombea Urais mmoja ambaye
atachuana na Yule ambaye atapitishwa na CCM.
Kwa kambi ya upinzani sina tatizo napo sana na
huenda wao wakawaleta wale wale wa miaka yote ambao wamekuwa wakigombea, nahapa
tunataraji majina kama ya Ibrahim Lipumba, Dk Wilbrod Slaa, Freeman Mbowe, Dk
Emmanuel Makaidi au hata Joseph Mbatia akaingia kwa mara ya kwanza.
CCM naweza kusema kuwa ndio watako tupa picha
halisi ya uchaguzi wa mwaka huu kwa ngazi ya Urais utakuwaje. Hii ni kutokana
na chama hicho kuwa na watu wengi ambao wanaweza kupitishwa na changamoto
wanayokabiliana nayo mwaka huu ndani ya CCM basi naimabni wao wakimaliza
uchaguzi wa nani agombee urais basi
watakuwa wamemaliza kazi na huko mbele watakuwa wanateleza tu na watabaki na
vita ya ubunge.
Kubwa ambalo nataka kulisema hii leo ambalo
limenijia katika mawazo yangu na kiukweli ni jambo la muhimu, ni kuacha siasa
za maji taka.
Naamini wapo wagombea ambao watatumia lugha zisizo
faa na ambazo hazikubaliki katika majukwaa ya kiasiasa. Hizi ni ni zile siasa
za kuchafuana ambazo zinawafanya wagombea kuacha kujinadi kwa sera zao ambazo
zitatupa ushawishi wa kumpigia kura na badala yake anatumia muda mwingi kutukana
na kuwaponda kwa kashfa za kila namna.
Si vyema kutumia muda wako mwingi kujinadi kwa
kumchafua mwenzako, maana mbali na kuzungumza majukwaani lakini teknolojia ya
sasa inaturuhusi kushawishi wapiga kura wakowakuone bora zaidi hata kwa njia ya
mtandao.
Sio wagombea tu lakini hata na sisi ambao tumeunda
makundi au kambi kwaajili ya kumsaidia mgombea fulani ili ashinde basi tuwe
wastaarabu na tuache kutumia lugha za matusi na kejeli zisizo kuwa na maana na
zingine kukosa maadili ya kitanzania.
Tusitumie uhuru wetu wa kupashana na kupata habari
kwa kupitiliza, uhuru huu unaweza kututia matatizoni kwani tayari Sheria ya
Mkosa ya Mtandao 2015 imesha pitishwa na inaweza kutugharimu kama sio
wanasiasaa basi wafuasi kutokana na lugha na posti zetu katika mitandao ya
kijamii.
Leo hii ikupita katika mitandao ya facebook,
Twitter, blogs na WhatsApp utashuhudia baadhi ya watu wakitoa kashfa na maneno
tofauti ya kuwaponda watu fulani fulani waliotangaza nia au waliona matarajio
ya kutangaza nia ya kuwania uongozi fulani.
Nadhani jambo jema la kufanya hivi sasa ni kutumia
mitandao hii ya kijamii, na hata vyombo vingine vya habari kwa ufasaha na
umakini kwa kunadi sera na mipango thabiti ya wagombea wetu tunaowataka na muda
mwingi tuwanadi wao na si kutumia kwa kutoa kashfa na kejeli kwa mgombea
mwingine ambaye unaanika mabaya yake tu kana kwamba yeye hana zuri hata moja
hapa duniani.
Wagombea pia nanyi wahimizeni wafuasi wenu kuwa
watulivu katika kipindi hiki cha kuelekea kupata wagombea, amani na upendo liwe jambo jema la kusisita kila
iitwapo leo maana bila hiyo ahata hilo tunalolitaka halitakuwa na raha.Porojo hii imetoka katika gazeti la HABARILEO toleo la Mei 29,2015 kama WAZO.
0 comments:
Post a Comment