Picha ya Pamoja
Wakuu
wa taasisi za kuzuia Ruswa barani Africa wamekutana katika ukumbi wa
mikutano AICC katika kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia
malengo ya kutokomeza Rushwa ndani ya Bara La Africa.
Wakuu hao
ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa
barani Afrika AUABC iliyopo chini ya jumuia ya muungano wa nchi za
Afrika ambapo mwenyekiti wa Taasisi ya AUABC Jaji Daniel Batidam amesema
kuwa wanatarajia kwa mkutano huu utasaidi kupunguza makali ya Ruswa
ndani ya bara hili.
Amesema kuwa kiwango kikubwa wanaangalia jinsi
gani wataweza kuondoa ruswa katika taasisi za jamii kwa maana ndio
zinazochangia kwa kiasi kikubwa maenbdeleo ya nchi zetu za kiafrika.
Pamoja
na hayo amesema kuwa tatizo kubwa la Rushwa ndani ya bara la Afrika ni
mfumo uliopo ambao unakuwa unaweka mianya ya rushwa pamoja na hayo
alisisistiza kwa wananchi kuacha kutoa rushwa ili kuiondoa kabisa.
Bodi hiyo imeundwa na watu 11 kutoka nchi mbalimbali barani Africa




0 comments:
Post a Comment