Mkuu
wa kitengo cha Biashara Maxcom Africa Bw. Deogratius Lazari (Katikati)
Akifafanua Jambo kwa waandishi wa habari ambao hawapo katika picha wakati wa
Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutoa huduma za Maxmalipo kwa kutumia simu ya
kiganjani, wengine katika picha ni
Maasifisa wa Kampuni Kulia msimamizi mauzo na Usambazaji kanda ya
mashariki Bwan Bw. Thomas Mwakalembile na Geofrey Mwakamyanda
Maxcom
Africa maarufu kama MaxMalipo ni kampuni ya kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2010
ambayo imewekeza katika kurahisisha maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla
kiuchumi na kijamii kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano (ICT
Technology).
Ili
kufikia malengo na Sera ya Taifa ya kutumia mifumo ya kielekroniki kutoa huduma
na pia kuwezesha Watanzania walio wengi kufikiwa na huduma hizi (Financial
Inclusion) na pia kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuongeza
ajira, MaxMalipo imeanzisha huduma mpya
itakayomuwezesha mtanzania kulipa bili zote kwa kutumia simu ya kiganjani aina ya
Smart phone yenye Mfumo utakaojulikana kama SmartMalipo.
Huduma
hii inatarajiwa kutoa ajira kwa watanzania takribani laki mbili (200,000) nchi nzima kufikia mwaka 2016 na hivyo kuchangia ukuaji wa sekta isiyo rasmi
ya ajira na kunyanyua uchumi wa Nchi.
Mfumo huu utaweza kurahisisha ulipaji wa bili mbalimbali Mfano; Umeme
(Luku), Ving’amuzi vya Televisheni, Vocha za Mitandao yote, Kulipia Kodi za TRA
na Baadae Kufanya Miamala ya Kibenki inayohusisha Kuweka na Kutoa fedha, huduma
ambazo kwa sasa zinalipwa kupitia mashine za MaxMalipo.
Huduma
hiyo inapatikana kwenye mfumo wa simu ya kiganjani ambapo mtumiaji atalazimika
kuweka mfumo wa SmartMalipo (Download
Smart Wakala Application) kutoka tovuti ya Google play au tovuti ya Maxmalipo
kwa kuandika neno ‘SmartMalipo au Maxmalipo’. Kisha mtumiaji atapata
maelekezo ya jinsi ya ku-install mfumo huu
kwenye simu yake na jinsi ya kutumia. Mfumo huu utamwezesha mtumiaji yeyote kuwa
Wakala na kulipia huduma zilizo orodheshwa. Mtumiaji
wa mfumo huu atajipatia kamisheni kama alivyo wakala
mwingine wa Maxmalipo kwa Huduma atakazofanya.
Watumiaji
wa mfumo huu wa SmartMalipo watatambulika kwa jina la ‘Smart Wakala’ popote
walipo na kufanya biashara kupitia simu zao za kiganjani. MaxMalipo
imeanzisha huduma hii mpya kwa lengo la kuwawezesha watanzania walio wengi
kufikiwa zaidi na huduma za malipo kwa
haraka wakiwemo wafanyabiashara wadogo na wenye mitaji midogo ambao kwa mazingira yao ni vigumu kuwa na
Mashine za Maxmalipo.
MaxMalipo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kupunguza matatizo ya foleni kwenye malipo ya huduma mbalimbali kama bili za
TRA, LUKU, DAWASCO, huduma za kibenki na hata katika mifuko ya Hifadhi ya jamii
Mfano PSPF.
Mwisho
kampuni ya Maxcom Africa - Maxmalipo inatoa rai kwa watanzania hasa
wafanyabiashara kuchangamkia huduma
zinazotolewa na kampuni hii ili kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia
katika mifumo ya utoaji huduma.
0 comments:
Post a Comment