Nafasi Ya Matangazo

May 18, 2015

New Picture (10)
Kikundi cha vijana 40 kiitwacho Wajenzi Isoso Wilayani Kishapu kikiendelea na ufyatuaji matofali ya kufungamana wakati kilipotembelewa na Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya kwa nia ya kuhakiki kazi wanazofanya. Halmashauri ya Wilaya hiyo imewapa vijana maeneo ya kufanyia kazi na mtaji wa kufanyia kazi zao.
New Picture (13)
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akiwa katika eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga maarufu kwa ajili ya vijana wa Juakali wanaotengeneza matofali ya kufinyanga na kuchoma, ambapo aliendesha zoezi la kukinyang’anya mashine iliyotolewa na NHC kama msaada kikundi cha vijana cha Amanias katika Manispaa hiyo baada ya kugundua kuwa kikundi hicho kimeacha kutumia mashine hiyo na kujiunga na kazi za juakali za kutengeneza matofali ya udongo wa kufinyanga.
New Picture (14)
Wakufunzi wa VETA Shinyanga wakiwa eneo la Kata ya Usanda wakimueleza Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya namna wanavyoshiriki kurekebisha hitilafu ndogondogo zinazojitokeza katika mashine za vijana za kufytatua matofali yanayofungamana alipokagua vikundi vya vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
New Picture (24)
Ofisa Miliki wa NHC Bw. Rockussy Sanka na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Bw. Muungano Saguya wakikagua ubora wa matofali yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana cha Tujiajiri na Miti ni Mali Wilayani Nzega.
New Picture (26)
Meneja waHuduma kwa Jamii na Meneja wa Mkoa wa Singida wakiwa katika Halmashauri ya Ikungi kuhakiki shughuli za vijana za kutengeneza matofali yanayofungamana. Vijana hao wameshajenga jingo la Ofisi yo ya kuendeshea kazi zao. PICHA ZAIDI: FK MATUKIO
Posted by MROKI On Monday, May 18, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo