Toka kushoto ni Kathrin Hoff, kijana Paulo, Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu.
Taasisis ya Imetosha ya jijini Dar es Salaam leo hii imepeleka misaada mbali mbali katika kijiji cha watoto wasioona cha Buhangija, Shinyanga ambacho kwa sasa kinahifadhi pia watoto na vijana wenye ualbino takriban 300.
Akiongea na watoto na vijana hao Mwenyekiti Masoud Kipanya alisema
taasisi hiyo inaangalia jinsi ya kutengeneza mazingira kwa kituo hicho
kujijengea uwezo wa kujipatia chakula badala ya kutegemea wasamaria wema
huja pale watakapojisikia wakati watoto katika kituo hicho wanahitaji
kula kila siku.Misaada hiyo ikiwemo mabelo ya mitumba 2 moja la masweta na jingine la suruali za jeans, unga, mchele, maharage, sukari, chumvi, ndoo 3 za mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia box 8, vile vile box 3 za vifaa vya hedhi vitakavyodumu miezi miwili pamoja na nguo za ndani dazeni 12 vyote hivo imegharimu Tsh milioni mbili na elfu sitini(2,060,000) ambazo zimetolewa na wanachama wa taasisi hiyo iliyojikita kupambana na mauaji ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu.
Mkuu wa kituo hicho alisema
anashukuru taasisi ya Imetosha kwa kuonesha mapenzi ya dhati na watoto
wa kituo hicho na kuguswa na changamoto zinazowakuta, kwani si mara
nyingi sana watu au taasisi kurudia kupeleka misaada kituoni hapo kitu
ambacho Imetosha wamekifanya. Wiki 3 zilizopita taasisi hiyo ilipeleka
msaada wa chakula kituoni hapo.
Awali mtafiti wa masuala yahusuyo watu wenye ualbino mJerumani Bi Kathrin Hoff alielezwa
kufurahishwa na jitihada zinazooneshwa na Imetosha kwa uhamasishaji
inayoufanya kwa jamii ya Ki Tanzania, pia amepongeza sana hatua ya
Imetosha kutaka kukifanya kituo cha Buhangija kujitegemea badala ya
kubaki tegemezi kama ilivyo sasa. Kathrin Hoff ni mhitimu toka chuo
kikuu cha Mainz nchini Ujerumani.
|
Hapa wakimsikiliza Masoud Kipanya |
Baadhi ya wasichana wa kituoni hapo wakifurahia msaada wa nguo za ndani na vifaa vya hedhi walivyokabidhiwa na mjumbe wa Imetosha aishiye Shinyanga Bibi Herriet |
Picha na habari kwa hisani ya TBN kanda ya kati.
0 comments:
Post a Comment