Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Arusha,Feruz Bano
akimkabidhi kitabu cha kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea aliyetangaza
nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Arusha mjini,Kim Fute jana ofisini
kwake mara alipofika kujitambulisha na kutangaza nia.
*********
Moses Mashalla,
Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Arusha kimetoa onyo kwa wagombea waliojitokeza kutangaza nia
ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupiti chama hicho kuacha tabia ya kuchafuana
na kuanza kampeni kabla ya muda.
Onyo hilo lilitolewa mwishoni mwa
wiki iliyopita na katibu wa chama hicho wilayani Arusha,Ferooz Bano wakati
akimkabidhi kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea alliyetia nia ya kugombea jimbo
la Arusha mjini kupitia chama hicho,Kim Fute .
Mgombea huyo alifika mbele ya ofisi
za CCM wilayani hapa kujitambulisha na
kutia nia ambapo mbali na kufanyiwa ukaguzi wa kadi zake za uanachama pia alikabidhiwa
kitabu chenye kanuni hizo na kupewa agizo la kutoshiriki kampeni kabla ya muda.
Hadi sasa jumla ya wagombea saba ambao ni Kim Fute,Phillemon Mollel”Monaban”, Mustapha Panju” Bushbuck”, Victor Njau,David Rwenyagira,Deo Mtui,Francis Laiser pamoja na
mbunge mstaafu wa jimbo la Arusha mjini,Felix Mrema wamejitokeza kutia nia
kuwania jimbo la Arusha mjini.
Akizungumza mara baada kumkabidhi
kanuni hizo katibu huyo wa wilaya aliwataka wagombea wote waliojitokeza kutia
nia kupitia chama hicho kuacha tabia chafu ya kupakana kuandaa sherehe kwa
wapiga kura.
“Muda wa kampeni bado haujafika
hatutaki nyinyi wagombea muanze
kuchafuana huko mitaani na wala kuandaa vijisherehe”alisema Bano
Hatahivyo,kwa upande wake mgombea
huyo mbali na kushukuru mapokezi ofisini hapo pia alihaidi kufuata maagizo ya
chama hicho na kusisitiz kwamba atafuata maagizo ya kanuni hizo kwa umakini
mkubwa.
Fute,alitangaza rasmi kuinga katika
kinyang”anyiro hicho kupitia CCM huku akijitapa kwamba amejipima na kubaini
anatosha kuwa mwakilishi wa jimbo la Arusha mjini kwa kuwa amegundua kuna ombwe
la uongozi.
0 comments:
Post a Comment