Naibu
Katibu Mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) Ezekiah Oluoch
akizungumza juu ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kitaifa utakaofanyika
Mei 28 katika mkutano Mkuu wa chama hicho utakaofanyika Mei 25 mpaka 28
katika ukumbi wa mikutano wa Ngurudoto,katika mkutano wake na waandishi
wa habari jana uliofanyika katika ofisi za mkoa za chama hicho,kushoto
ni Katibu wa chama mkoa Hassan Said.
*******
Chama
cha Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa kitaifa
May 28 mwaka huu ili kupata viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa
kipindi cha miaka 5 pamoja na kutetea maslahi ya walimu.
Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho Ezekiah Oluoch amesema kuwa nafasi
zinazogombaniwa ni Mwenyekiti wa chama,Katibu,Naibu Katibu mkuu pamoja
na Mhazini wa chama hicho.
Ezekiah
alisema hayo jana akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za
chama hicho Mkoa wa Arusha kuwa hadi sasa wana jumla ya wanachama 452
wamejitokeza kugombea nafasi hizo na nafasi nyingine ikiwamo Mwakilishi
wa Walimu wenye ulemavu ,na kitengo cha Walimu wanawake.
“Wagombea
ni wengi na nafasi ni chache tumeona tuache hivyo maana yake tukizuia
idadi tutakua tumeminya demokrasia” Alisema Ezekiah
Ezekiah
amesema kuwa jumla ya walimu 1000 wanatarajia kushiriki uchaguzi huo
wa kitaifa ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti
wa Chama hicho Mkoa wa Arusha (CWT) Jevin Buruya amesema kuwa
wamejiandaa vyema kwa ajili ya uchaguzi huo hivyo amewataka walimu
wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi huo.
Jevin
amesema kuwa Chama cha Walimu Tanzania kitafanya mkutano mkuu
utakaoanza May 25 hadi 28 ambapo agenda kuu ni Uchaguzi Mkuu,Mkutano huo
unatajwa kuwa Mkutano wa Mwisho wa Raisi Kikwete kuwahutubuia walimu . Source: Habari picha Na Ferdinand Shayo,Arusha wa jamiiblog.
0 comments:
Post a Comment