Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma. SACP David Misime |
WATU wanne wamepoteza maisha jana Aprili 10 mwaka huu badaa ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya Nyahunge lenye namba za usajili 506 CSX Youtong kugongana uso kwa uso na gari lenye
namba za usajili T. 856 ALM Toyota Mark II katika eneo la Nzuguni barabara kuu ya Morogoro Dodoma.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, SACP David Misime amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali ni dereva wa gari dogo aliyeingia barabara kuu bila kuchukua tahadhari.
Kamanda Misime amewataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni:-
1.
JACKSON LAZARO,
mwenye miaka 51, Askari wa JWTZ Monduli Arusha na Mkazi wa Nzuguni aliyekuwa akiendesha gari dogo.
2.
HELENA MICHAEL CHIUYO, miaka 36 na mkazi wa Makole.
3.
FATUMA PATRICK
MTAUGA, miaka 17, Mwanafunzi Kidato cha Tatu City Sekondari na mkazi wa Makole.
4.
STELLA BATON
GIDEONI, mwenye miaka 35 mkazi wa Kisasa.
Ajali
hiyo ilitokea katika makutano ya barabara inayotokea Kijijini Nzuguni, ambapo
dereva wa gari ndogo alikuwa akitokea kijijini Nzuguni kuingia barabara kuu ya
Dodoma/ Morogoro na kugongana na Bus ambalo lilipoteza mwelekeo na kuingia
porini umbali usiopungua mita 300 na kugonga mti kisha kusimama. Katika Bus
majeruhi wawili walipata michubuko kiasi na walitibiwa katika Hospitali ya Mkoa
wa Dodoma na kuruhusiwa.
Chanzo
cha ajali hiyo ni dereva wa gari ndogo T. 856 ALM Toyota Mark II kuingia
barabara kuu bila kuwa makini na kusababisha kushindwa kumpa kipaumbele aliyekuwa
barabara kuu kupita kwanza lakini pia mwendo kasi wa dereva wa bus kumesababisha
madhara kuwa makubwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME –
SACP ametoa wito kwa madereva pamoja na wanaosomea udereva, kufuata sheria za
usalaba barabarani, wanapaswa kila mara kuzingatia udereva wa kujihami kwamba
ninapoendesha gari linaweza kutokea jambo lolote lile mfano dereva mwenzangu
kukosea, mtembea kwa miguu kukatisha ghafla nk.
Je, kwa mwendo huu nitaweza
kusimama bila kuleta madhara? Hata kama nikishindwa madhara yasiwe makubwa,
busara na kutokulipiza kisasi.
0 comments:
Post a Comment