Afisa masoko wa Airtel tanzania Prospa Mwanda akionyesha kwa wanafunzi
wa chuo Kikuu dodoma (UDOM) jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi Intaneti
inavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo chuoni hapo
jana. Airtel Tanzania chuoni hupo imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana
kwa wananfunzi kwa gharama nafuu
Afisa masoko wa Airtel tanzania Prospa Mwanda akionyesha kwa wanafunzi
wa chuo Kikuu dodoma (UDOM) jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi Intaneti
inavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo chuoni hapo
jana. Airtel Tanzania chuoni hupo imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana
kwa wananfunzi kwa gharama nafuu
Meneja
masoko wa Airtel Uni Wi-Fi Bi Aneth Muga anaepiga picha ya selfie ili
waitume kwa kutumia huduma ya Airtel Wi-Fi intaneti kwa baadhi ya
uongozi wa wanafunzi na mshauri wa wanafunzi chuoni hapo mara baada ya
Airtel kuzindua huduma yao ya intaneti Wi-Fi yenye kasi zaidi maalum
kwa wanafunzi wa chuo hicho jana.
Mshauri
wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) bw, Dick Manong akiongea
na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya
Airtel UNI Wi-Fi jana chuoni hapo ambapo itawasaidia wanafunzi kupata
intaneti kwa gaharama nafuu ya yenye kasi zaidi.
kutokana na ukweli kwamba Dodoma ni mji
mteule na wenye kuendelea kwa kasi hapa nchini na pia ni mji uliobahatika kuwa
miongoni mwa mji wenye chuo kikubwa hapa Tanzania, Airtel Tanzania mkoani huko imezindua
huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa
wananfunzi kwa gharama nafuu
UNI WI-FI itawezesha
wanafunzi zaidi ya 60,000 katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupata huduma ya
kimtandao ya Intaneti iliyo bora na nafuu pamoja na kukidhi mahitaji ya wote waishio chuoni hapo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mkurugenzi wa
huduma kwa wateja Airtel Bi , Adriana Lyamba alisema: "Leo hii tunazindua
Airtel UNI WI- FI huduma ya internet inayopatikana kwa bei nafuu kwa ajili ya
wanafunzi na pia tumeongeza mnara wa pili wa simu ambao
tunaamini utaimarisha mtandao wetu hapa UDOM na kuinua uchumi wa nchi
yetu na kwa watu wanaoishi karibu na maeneo haya "
Tunafuraha
kubwa kwa Airtel kuweza kuboresha Maisha ya wanafunzi hapa chuoni kwani
spidi hii itawawezesha wanafunzi kuweza kufanya utafiti wao, kupata habari
mbalimbali za taaluma au kijamii kupitia mtandao wetu wa Airtel
"
Meneja Masoko wa
Airtel UNI WI-FI, Bi, Aneth Muga, alisema "Airtel wifi itakuwa inapatikana
kwa mwanafunzi yoyote hapa UDOM, kwa kutumia simu zao za mkononi, laptop,
kamera na kwa mwanafunzi yoyote aliyepo UDOM bila kujali mtandao wa simu
wanaoutumia.
Wanaweza
kununua UNI Wi-FI vocha ambayo inapatikana masaa 24 , kwa kifurushi cha siku , wiki, mwezi na kifurushi cha usiku mzima.
Fikiria!
Unaweza kufurahia kifurushi cha 1 GB kwa shilingi 500 tu! Alisisitiza Bi, Muga
Kwa upande wake
mgeni rasmi ambae ni mshauri wawanafunzi chuoni hapo (UDOM) Bw, Dick Manongi alisema: ". Tunawashukuru sana Airtel
Tanzania kwa ajili ya uzinduzi wa huduma hii kubwa na ya bei nafuu hapa chuoni.
Nina hakika kwamba, huduma hii itaimarisha uwezo wa kujifunza na kuendelezea
wanafunzi urahisi wa kujipatia Habari mbalimbali zinazoendelea hapa
nchini na hata nje ya nchi ".
Ningependa
kuwaomba wanafunzi wote kutumia fursa hii kubwa ili kuweza kuongeza ujuzi wao
kitaaluma na katika Maisha yao ya baadae.
Uzinduzi wa
Airtel Uni Wi- Fi katika chuo kikuu cha Dodoma umekuja mara baada ya Airtel
Tanzania kuzindua huduma kama hiyo katika chuo kikuu cha Saint Augustine (SAUT)
jijini Mwanza na mipango mingine inaendelea kufikia vyoo vingine hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment