Kikosi cha FFU Oljoro ambacho kitashuka kuchuana na Tanzanite SC .
Mkoani
Arusha mwishoni mwa juma hili kunataraji kufanyika michuano ya NDONDO
CUP itakayoshirikisha jumla ya timu nane kutoka mkoani hapa.
Lengo
la michuano hiyo ni kuwakutanisha wapenda soka mkoa wa Arusha pamoja na
kuwapa nafasi wa mashabiki wa mchezo huo Mkoani hapa kukutana sehemu
moja.
Michuano hii itaanza kutimua vumbi siku ya Ijumaa ya tarehe 24/04/2015 na kufika tamati siku ya jumapili.
Mshindi
wa kwanza katika michuano hii atapata zawadi ya fedha taslimu shilingi
laki tano (500,000) pamoja na kikombe, mshindi wa pili atajipatia fedha
taslimu shilingi laki tatu (300,000).
Timu
zitakazoshiriki katika michuano ya NDONDO CUP 2015 ni FFU OLJORO,
TANZANITE SPORTS FOUNDATION, RED STAR, TANZANITE VETERAN, LEMARA BOYS,
NJIRO SPORTS, SMALL NYOTA na UMBRELA GARDEN.
Ratiba katikIMA MICHUANO HIYO NI KAMA IFUATAVYO
FFU OLJORO VS TANZANITE SPORTS CLUB, TANZANITE VETERAN VS RED STAR, LEMARA BOYS VS UMBRELA GARDEN, NJIRO SPORTS VS SMALL NYOTA
Michezo
yote itapigwa siku ya ijumaa kwa mfumo wa bonanza na nusu fainali
itakuwa siku ya jumamosi wakati mchezo ya fainali utapigwa siku ya
jumapili.
Michuano
hii itafanyika katika uwanja wa AICC uliopo karibu na round about ya
KIJENGE. muda ni kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 12 jioni.
Katika
michuano hii kutakuwa pia na burudani toka kwa bingwa wa kucheza na
baiskeli dunia (BMX CHAMPION) VICK GOMEZ, pamoja na wasanii wa Bongo
flava akiwemo G NAKO, CHABA, KINGS, na mchekeshaji KATARINA.
0 comments:
Post a Comment