DAUDI MRINDOKO KASHAWISHIKA NA KAKUBALI OMBI LA WANANCHI WA JIMBO LA MOSHI MJINI KUGOMBEA UBUNGE 2015
"Kwa nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu anawezesha yote na kutujalia uhai
Waheshimiwa
Mabibi na mabwana,vijana na wazee,watoto na wakubwa ,Baba zangu na mama
zangu na wanadau wote wanaoishi Moshi na wenyeji wa Moshi walio ndani
na nje ya Moshi.
Mimi mtoto wenu,mdogo wenu na Kijana wenu DAUDI BABU MRINDOKO
Nina
heshima kubwa na unyeyekevu kwenu ,Pia nawashukuruni sana kwa
kunishawishi niweze kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge wa jimbola Moshi Mjini katika uchaguzi mkuu 2015,nafasi ambayo Ubunge ! ambayo mimimwenyewe kwa tafsiri ya Ubunge yaani utumishi,mtetezi,msemaji, mwakilishi n.k
Katika
baraza la kutunga sheria na katiba yaani Bunge, na katika tafsiri hii
ya majina ya kazi hii lazima mtumishi awe mkweli,muwazi na aliyeweka
mbele kwanza maslahi ya walio mchagua.
Waheshimiwa Mabibi na mabwana,vijana na wazee,watoto na wakubwa ,Baba zangu na mama zangu Kunishawishi kwenu Kulinifanya niwe kimya kiasi na nikiwa najiuliza maswali mengi kichwani ! Lakini maswali makubwa yalikuwa 3 (a) Nashawishiwa na jamii nichukue fomu kwa kuwa mimi ni kijana mwenywe uwezo wa kuifanya kazi hii?
(b)Nashawishiwa
kwa kuwa kijana niliozaliwa na kuelimishwa na wanao nishawishi? yaani
wanachi wa Moshi mjini na ndio wananitambua tabia na uwezo wangu wa
kikazi.
Swali lingine nililojiuliza ni:
Hivi mtoto au kijana mwenye adabu ,Nidhamu na heshima kwa wazee na
wakubwa zake walikuwa katika jamii wakimteua au kumtuma kufanya kitu au
jambo tena kwa faida na maslahi ya jamii,itakuwa vema kijana huyo
akatae? au asikubali kutumwa huko?
Baada ya kujiuliza mashwali hayo na mengineyo nimepata jibu ambalo:
NAKUBALI WITO WENU NA USHAWISHI WENU
Kuwa nitachukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge 2015 jimbo la Moshi Mjini.
Mmenishawishi nami nashawishika na kuthubutu kuchukua fomu ya kugombea ubunge,kwa kuwa siwezi kuwa mvunjifu au mtovu wa adabu kukataa wito na ushawishi wenu ambaowazee wangu,vijana wenzangu,mama na baba zangu wa Moshi mjini mmeniteua kwa kunishawishi niweze kuja kuwa mtumishi wenu mbunge.
Kwa kuwa mmenizaa,mmenilea ,mmenisomesha mpaka elimu ya juuna mmenishawishi kwa kuwa mnaniamini mimi ni mmoja wenu katika maisha
ya kila siku katika jamii yetu Moshi,yanafahamu wazi mahitaji yetu,kero
zetu na kipi jamii yetu haitaki na kipi? Jamii yetu inataka hapa
jimboni Moshi Mjini,Marekebisho gani ?yanatakiwa hapa Moshi mjini ili palete tumaini jema na maana kamili wa wakazi wote jimboni hapa Nayafahamu yote.
Nanyi mmemshawishi Kijana Daudi Babu Mrindoko,mtoto wenu kwa hakika mmetuma mtumishi anayeguswa na yanayowagusa, anayekerwa na yale mnayokelwa ! anafurahishwa na yale mnayofurahia Kwa ni mwenzenu katika jamii jimboni Moshi mjini.
Nawashukuruni sana na Asante sana kwa Kunishawishi,Nimeshawishika Nangojea wakati ukifika nami nifuate taratibu zote za kuchukua fomu kupitiaChama tawala"
"NAKUBALI NITACHUKUA FOMU 2015,KWA NIA YA USHIRIKIANO WETU TULETE MABADILIKO MOSHI MJINI YENYE MASLAHI KWA WOTE"
Mungu Ibariki Tanzania
0 comments:
Post a Comment