Nafasi Ya Matangazo

April 15, 2015

 Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Lilian Festo Mjimba katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman (kulia), akikabidhi mfano wa funguo za gari jipya aina ya Toyota IST, kwa mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Kinyozi Juma Ally Songoro katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.
*************
Airtel yakabithi magari kwa washindi 8 wa Mkoa wa Dar es saalam Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabithi magari kwa washindi wake waliokuwa wamesalima kwa mkoa wa Dar es saalamu walioibuka washindi katika droo za mwisho za promosheni ya Airtel yatosha zaidi.

Washindi waliokabithiwa magari yao ni pamoja na  kuruthumu Seleman (42) mfanyabishara ndogondogo, Lilian Mgimba (24) mfanyabishara ndogondogo, Christ Mbalamula (27) mjasiliamali , Juma Songoro(24) Mwanafunzi wa chuo cha IFM , Subeti Salum Subeti (43) kondactor wa daladala, Isgnenia Mushi(35) mfanyabishara ndogondogo,Charles Msakwa
(45) Mwalimu, na  Obed Muamugija (24) Mwanafunzi wa chuo cha IFM.
 

Akiongea wakati wa kukabithi magari hayo Mkurugenzi wa kitengo cha teknolojia habari wa Airtel Bw, Frank Filman alisema “ nawashukuru sana wateja wetu kwa kutumia huduma zetu hususani huduma ya Airtel yatosha zaidi ambayo mbali na kuwazawadia wateja wanaotumia vifurushi kupitia promosheni ya Airtle Yatosha zaidi tumewawezesha wateja wetu kupata huduma bora, za nafuu zinazokithi mahitaji yao ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi pamoja na huduma ya internet.
 
Leo tunajifuraha kukabithi magari kwa washindi 8 waliosalia katika mkoa wa Dar es saalam, tunawaahidi washindi wengi waliosalia kutoka kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa kuwa watakabithiwa magari yao ndani ya wiki moja kuanzi sasa.

Tunawapongeza wateja Wetu wote waliobahatika kujishindia magari kupitia promosheni hii tangu ianze na tunaamini tumeweza kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii na za kiuchumi kwa urahisi zaidi na kuboreesha maisha yao na jamii ya Tanzania kwa ujumla
Tunawaahidi kuendelea kutoa huduma za mawasiliano bora, zenye ubunifu huku tukiendelea kuwafikia watanzania wengi zaidi na kuwazawadia kupitia promosheni kama hii ya Airtel Yatosha Zaidi.

Promosheni ya Airtel yatosha imeshafikia mwisho wake lakini huduma yetu ya Airtel yatosha bado inaendelea hivyo natoa wito kwa watanzania kuendelea kujiunga na vifurushi hivi na kufurahia huduma bora zenye gharama nafuu kwa wakati wote. aliongeza Filman.

Kwa upande wake moja ya washindi wa promosheni hii bi, Kuruthumu Seleman alisema” mpaka sasa sijaamini kwamba nimeshinda gari, kwakweli nawashukuru sana Airtel kwa kuanzisha promosheni hii. Kwakweli sikuwa na wazo kama naweza kushinda, haya ni maajabu kwakeli kumbe kila mtanzania anaweza kupata nafasi ya kushinda kupitia promosheni hizi za Airtel.

Nafurahia ushindi huu kwa sasa kwani nilikuwa natamani kuwa na usafiri na kupunguza adha nayoipata katika shughuli zangu za mama lishe, sasa nauhakika wa kusafirisha chakula changu kwa usalama zaidi na kuwafikia wateja wangu kwa wakati, naamini biashara yangu itaboreshwa na kukua na kuwa ya ufanisi zaidi sasa kulinganisha na  ilivyokuwa awali”
 
 
Promosheni ya Airtel yatosha ilizindualiwa mwanzoni mwa mwezi wa februari mwaka huu na kufika mwisho wake mwanzoni mwa mwezi Aprili ambapo  jumla ya  wateja 60 wamejishindia na kukabithiwa magari yao aina ya Toyota IST. Airtel iliwazawadia wateja wake gari aina ya Toyota IST kila siku kwa muda wa siku 60
Posted by MROKI On Wednesday, April 15, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo