Nafasi Ya Matangazo

April 30, 2015

Kiongozi wa Nidhamu wa Timu za Michezo Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Samwel Mwashamba pamoja na baadhi ya wavuta Kamba wakifurahia makombe ya ushindi waliyojinyakulia wakati wa Michuano ya michezo ya Mei Mosi Jijini Mwanza Aprili 29. 2015.
Mchezaji wa kuvuta Kamba wanawake Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kisinza akipokea kombe la ushindi kutoka kwa Mgeni rasmi Bw.Hussein Baraka (Mwenyekiti wa Shirika la Madini la Taifa) baada ya Timu yao kuibuka nafasi ya tatu kwa kuzidiwa alama mbili na timu ya uchukuzi na Wizara ya Mamno ya Ndani Aprili 2015.
Mchezaji wa kuvuta Kamba wananume Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Salimu Mwokiwa akipokea kombe la ushindi kutoka kwa Mgeni rasmi Bw.Hussein Baraka (Mwenyekiti wa Shirika la Madini la Taifa) baada ya Timu yao kuibuka nafasi ya pili kwa kuzidiwa alama moja na timu ya uchukuzi, Aprili 2015.
Posted by MROKI On Thursday, April 30, 2015 No comments
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) nchini Tanzania Dkt.Albina Chuwa akifungua Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala la wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam. Kongamano hilo la siku 2 linajadili namna Bora ya uendeshaji wa Taasisi za Takwimu na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za masuala ya Takwimu Barani Afrika.
Mtendaji Mkuu wa  Taasisi ya  Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi  za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Takwimu Barani Afrika (AFRISTAT) pia mtaalam wa Takwimu kutoka nchini Cameroon Bw. Martin BALEPA akiwasilisha mada kuhusu namna nchi za Bara la Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kutumia takwimu sahihi.
 Andry Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la  watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za Afrika linalojadili masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania wenyeji wa mkutano huo.
Baadhi ya watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala linaloendelea jijini Dar es salaam.
Watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa la siku 2 linalojadili masuala ya Uongozi na utawala wa taasisi za takwimu Barani Afrika linaloendelea jijini Dar es salaam.
Posted by MROKI On Thursday, April 30, 2015 No comments

Mkurugenzi wa halmshauri ya wilaya ya Ruangwa, Nicholous Kombe (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 100 kwa Mwenyekiti wa WAALIMU SACCOS ya Ruangwa, Hamisi Malunga (kushoto)  ikiwa ni mkopo uliotolewa na mfuko wa pensheni wa LAPF kwa wanachama wa SACCOS hiyo. Katikati yao ni Meneja wa LAPF, Kanda ya mashariki, Yessaya Mwakifulefule pamoja na wanachama wa Saccos hiyo wakati wa mabidhiano hayo juzi Wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Wanachama wa  Walimu Saccos wa Wilaya  ya Ruangwa mkoani Lindi wakifurahia   mkopo wenye thamani ya shilingi Milioni 100 uliotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa wanachama wa Saccos hiyo. Anaeshuhudia wa pili kulia ni Meneja wa LAPF,  Kanda ya Mashariki, Yessaya Mwakifulefule. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Wilayani Ruangwa hivi karibuni.
***************
Mfuko wa pensheni wa LAPF leo umetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni mia moja kwa Saccos ya waalimu iliyopo wilayani ruangwa mkoani Lindi.

Akipokea hundi ya mkopo huo kwa kwa niaba ya wanachama wa Waalimu Saccos,mkurugenzi wa halmshauri ya Ruangwa Bw Nicholous Kombe aliishukuru mfuko wa LAPF kwa kuwajali na kuwawezesha wanachama wa SACCOS hiyo ambao walikua wakiuhitaji sana mkopo wa aina hiyo.

Akishukuru kwa niaba ya waalimu wanachama wa saccos hiyo,Mwenyekiti wa saccos Bw Hamisi Malungu aliwaomba wanachama wake wadumishe nidhamu na kuheshimu kulipa mikopo yao kwa wakati ili Saccos yao iweze kukopesheka Zaidi.

Nae Meneja wa LAPF kanda ya mashariki Bw Yessaya Mwakifulefule,aliwapomgeza wanachama wa SACCOS hiyo na kuwashauri waalimu wengi Zaidi wachague kuchangia makato yao kwa mfuko wa LAPF ili na wao waweze kufaidika na mikopo kama hiyo li waweze kuwajikwamua kiuchumi.

Aidha bwana Mkwakifulefule alisema mpaka sasa LAPF imesha kopesha Zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa saccos mbali mbali za wanachama ambao makato yao wanachangia ktk mfuko huo hapa nnchini.

Waalimu SACCOS ilianzishwa mwaka 2001 ikiwa na wanachama 60 ambapo mpaka sasa saccos hiyo ina wanachama Zaidi ya 300 na hisa zenye thamani ya shilingi 26,000,000.
Posted by MROKI On Thursday, April 30, 2015 No comments
Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya Alliance Insurance.
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi Fauzia Kullane.
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Godwin Gondwe
*******
KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.
Utafiti huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango  makao makuu nchini  Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko  na maoni ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.
Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000 zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya jsu  kwa mwaka wa 2015 -2016.
Posted by MROKI On Thursday, April 30, 2015 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo