Watu watatu wameuawa
Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti yanayohusisha imani
za kishirikina.
Tukio la kwanza limetokea
tarehe 01/03/2015 majira ya saa 01:00hrs katika kitongoji cha Golani, kijiji
cha Masinyeti, kata ya Iduo, tarafa
ya Mlali Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina
la SAIDIA S/O CHAKUTWANGA mwenye miaka
80, kabila Mkaguru, Mkulima Mganga wa kienyeji aliuawa na watu waliojichukulia
sheria mkononi kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kutobolewa macho.
Uchunguzi wa awali
unaonyesha chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina wakimtuhumu marehemu
kuwa anazuia mvua kunyesha katika eneo hilo.
Katika tukio lingine
limetokea tarehe 01/03/2015 majira ya saa 02:00hrs katika kitongoji cha Majengo, kijiji cha Ihanda, Kata na Tarafa ya
Mlali Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la PETER S/O KALULI mwenye miaka 85, kabila
Mkaguru akiwa na mkewe aitwaye KAILA
W/O KALULI mwenye miaka 80, Mkaguru wote wakulima na wakazi wa Kitongoji cha Majengo wakiwa wamelala
ndani ya nyumba yao ya tembe, waliuawa na watu wasiofahamika kwa kuangushiwa
ukuta wa nyumba yao kisha kuchoma moto na kubomoa nyumba mbili za tembe.
Watu hao walifanya
uharibifu mwingine kwa kuwaua nguruwe mmoja na ng’ombe mmoja kumkata miguu.
Uchunguzi wa awali
unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji na uharibifu huo ni imani za kishirikina wakiwatuhumu
marehemu kuwa wanazuia mvua kunyesha. Watuhumiwa wanne akiwemo M/Kiti wa Kijiji cha Ihanda na wazee
wawili wa kimila wa kijiji wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio
hili kwani taarifa zinaonyesha waliandaa vikao vya kutekeleza mauaji haya.
Upelelezi wa matukio yote mawili unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwatafuta
watuhumiwa wengine waliohusika na matukio haya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime – SACP ametoa wito
kwa wananchi kutochukua sheria mkononi
na kujiepusha na imani za
kishirikina zinazopelekea kuleta hofu na mashaka kwa jamii. Alisema ni jambo
la aibu kwa jamii hadi karne hii watu kuamini kuwa kuna watu wanaoweza kuzuia
mvua isinyeshe. Pia amewataka viongozi wa maeneo mbalimbali kutoa taarifa mapema
polisi pale wanapoona mipango ya kihalifu kama hiyo ikipangwa.
Imetolewa
na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
0 comments:
Post a Comment