Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
akishiriki usafi wa mazingira katika Mtaa wa Mlalakuwa na wakazi wa Mtaa huo
wakati wa operesheni maalum ya kuweka safi mazingira.
********
MPANGO
wa kuweka safi mazingira ya jiji la Dar es Salaam utafanikiwa tu iwapo viongozi
na watendaji watatekeleza mpango huo kwa vitendo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa operesheni
maalum ya kusafisha maeneo mbalimbali ya Kata ya Mikocheni, Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Yusuph Mwenda alisema umefika wakati sasa viongozi kchukua hatua za
makusudi za kuhakikisha mkakati wa kuweka safi jiji unafanikiwa kwa
kuwashirikisha wananchi wao kwa vitendo.
Mwenda
alithibitisha hilo kwa vitendo wakati alipojumuika na wananchi mbalimbali wa
Mtaa wa Mikocheni B, Manispaa ya Kinondoni kusafisha maeneo mbalimbali ya Mtaa huo ikiwemo sehemu za mto Mlalakuwa na
kuwahakikishia wananchi wake kuwa hilo litakuwa zoezi endelevu ili kuhakikisha
kila mwananchi anahamasika na kuweka safi mazingira yanayomzunguka.
“Kinondoni
imekuwa Manispaa ya kuigwa katika suala la usafi, na hili tunalitekeleza kwa
kujumuika na wananchi wenzangu kwa ajili ya kusafisha maeneo mbalimbali na leo
tupo Kata ya Mikocheni B. viongozi wanatakiwa waoneshe wananchi wao kwa
vitendo, nao watahamasika .” alisema Mwenda.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni akioneshwa sehemu
mbalimbali za Mto Mlalakuwa wakati wakiufanyia usafi.
Meya wa
Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwa kwenye picha ya pamoja na wakazi wa
Kata ya Mikocheni B baada ya kumaliza kufanya usafi katika mto Mlalakuwa.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa
pili kulia) akikabidhi viroba kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni
B, Sixbert Thomas kwa ajili ya kuzuia maporomoko ya ardhi katika Mto Mlalakuwa,
wakati wa operesheni hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
(kulia) akimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa,
Abraham Shoo (kushoto) wakati wa operesheni maalum ya kusafisha mazingira
katika Kata za Manispaa hiyom Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Nicodemus Masika.
0 comments:
Post a Comment