Kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania imeeleza kuguswa na tukio la mvua kubwa iliyonyesha wilayani
Kahama mkoani Shinyanga ambayo imesababisha vifo vya watu 42 na wengine mamia
kujeruhiwa na kuacha familia nyingi zikiwa hazina makazi na kuanzia leo imeanza
kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tukio hilo.
Akiongea na waandishi wa
habari leo,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa wa Vodacom Tanzania,
Rosalynn Mworia amesema anawaomba watanzania wote wanaotaka kuchangia wahanga
hao kutuma fedha zao kwenye namba
maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya 155990.
“Tukiwa kama kampuni ya
mawasiliano tumeguswa na tukio hili na tunawapa pole waathirika wote na
tunaungana na wakazi wa kahama kwa janga hili tutatoa mchango wetu wa hali na
mali kwa kupitia kitengo chetu cha kusaidia jamii cha Vodacom Foundation na tunawaomba
watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao na
tutahakikisha tunaifikisha sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu ambao wako
katika mazingira magumu na wanahitaji msaada wa haraka”.
Alisema kupitia njia hii ya
namba maalumu ya”Red Alert” 155990 ya kuchangisha fedha imewahi kurahishisha
uchangishaji wa fedha kwa waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na
kuathiri wananchi moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo
la mboto jijini Dar es Salaam na aliwahimiza wananchi kuitumia kama njia rahisi
ya uchangiaji.
Jinsi ya kuchangia ni rahisi
sana unachotakiwa kufanya unaponyeza *150*00# alafu unachagua namba 4 yaani
Lipa kwa M PESA baada ya hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni naweka namba 155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya
simu baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.
0 comments:
Post a Comment