Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto),
akizungumza na viongozi wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro (kutoka
kulia), Diwani wa kata hiyo, Yannick Ndoinyo, Mwenyekiti wa kijiji cha
Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili
Naing’isa, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini
Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo
kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa
na hapo awali.
Diwani wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro, Yannick
Ndoinyo, (kulia), akifafanua jambo kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), wakati baadhi ya viongozi
wa kata hiyo, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini
Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo
kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano
ikilinganishwa na hapo awali. Wa (wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa kijiji cha
Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili
Naing’isa.
0 comments:
Post a Comment