Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira James Lembeli akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Kamati
yake kwa Kipindi cha Mwaka 2014, Bungeni mjini Dodoma.
KAMATI ya Bunge ya Ardhi, Maliasili
na Mazingira imesema kuwa hatua za Serikali za kupambana na ujangili nchini zimeonesha
mafanikio makubwa.
Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa
Kazi za Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, James Lembeli alisema kuwa pamoja na
mafanikio mengine hatua hiyo imefanikiwa kukamata silaha 2000.
Alisema hadi kufikia mwaka
2013, hali ya ujangili wa tembo ilikadiriwa kufikia tembo 30 kwa siku, lakini
Serikali ilichukua hatua ya kuzuia na kutokomeza uhalifu huo kwa kuanzisha
Operesheni Tokomeza.
“Pamoja na madhara
yalijitokeza operesheni hiyo ilisaidia kuanza kupungua kwa kesi za ujangili wa
tembo nchini” alisema Lembeli.
Alifafanua kuwa baada ya
Operesheni hiyo Serikali iliendelea kuchukua hatua zaidi kwa lengo la
kutokomeza kabisa tatizo hilo.
“Hatua zilizochukuliwa ni
pamoja na kuajiri askari wa wanyamapori zaidi ya 500 na wengine 300 waliajiriwa
ikiwa ni askari wa kujitolea”alisema.
Hata hivyo aliishauri Serikali
kuendelea na harakati za kupambana kwa nguvu zote na ujangili na kuweka wazi hali ya ujangili nchini ili
wananchi na wadau wa hifadhi nchini waungane na Serikali.
0 comments:
Post a Comment