Nafasi Ya Matangazo

February 06, 2015

Pweza ni mmoja kati ya samaki wanaopendwa sana na wakaziwa pwani kutokana na utamu wake, pia virutubisho muhimu kwa afya alivyo navyo.

Zipo aina tofauti tofauti ya mapishi ya samaki huyu,yakiwamo yale ya kukaanga ,kuchemshwa na kupata supu na hata kupikwa kama mchuzi.

Ni imani ya wanaume wengi wa pwani na hata kutoka bara ambao huishi ukanda wa pwani siku hizi hupenda supu ya pweza kutokana na wingi wake wa virutubisho ambavyo huamini kuwa vinaongeza nguvu za kiume kwa waliopungukiwa.
Ulaji pweza na supu yake, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na vyakula hivyo.

Hii iliwahi kusemwa na Dk Cuthbert Maendaenda na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Miji mingi nchini kwa sasa nyakati za jioni kuna supu ya pweza na wakati mwingine ukipita Posta Mpya kuna vuijana utakutana nao wakiuza pweza wa kukaanga.

Hiyo haitoshi lakini pia wapo vijana wengi wanao uza karanga za kukaa nga na mbichi lakini wapo akina mama na dada zetu ambao hupita na makarai yaliyo na mihogo mibichi. 

Yote hii ukionekana unakula au kutafuna muhogo na kipande cha mbata baaaaasi watasema una jibusti.

Wapo wanao kula kwa starehe tu lakini wapo walio na imani hiyo ya kujibusti.
 
 Mchuuzi wa Pweza na dagaa kamba wa jijini Dar es Salaam akitembeza samamaki hao katikati ya jiji.
Mkazi wa dar es Salaam akila kitoweo cha Pweza. Ukweli utabaki palepale kuwa vyakula vingi vya bahari vinavirutubisho vingi kwa afya yako. Muhimu hapa ni kuangalia tu usafi wa namna vyakula hivyo vilivyo andaliwa na vinavyouzwa.
Posted by MROKI On Friday, February 06, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo