Na Fredy Mgunda,Iringa
SHIRIKA la kuhudumia
viwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa
limetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 229.9 kwa
wajasiriamali wa mkoa huo, katika kipindi cha July mpaka Desembea mwaka
jana.
Akizungumza na Blog hii,
Kaimu meneja wa SIDO mkoani Iringa,
Niko Mahinya alisema lengo la mkopo huo ni kuwawezesha wajasiriamali
wadogo
kupata mitaji, na kuinua uchumi wao ili waondokane na
umaskini.
Alisema mikopo hiyo
ilitolewa kwenye vikundi mbalimbali vya
wilaya zote za mkoa wa Iringa na wajasiriamali mmoja mmoja, ambao
kupitia SIDO
wamefanikiwa kiuchumi.
“SIDO
imekuwa ikitoa
mikopo kwa wajasiriamali kwa masharti naafuu tofauti na taasisi nyingine
za
kifedha ili na riba ndogo ili kukuza mitaji yao, ”alisema.
Alisema lengo la kutoa
mikopo hiyo, ni kuwasaidia
wajasiriamali na wananchi wasiokopesheka kwenye mabenki na taasisi
nyingine za
kifedha.
Alisema mikopo hiyo ni
rahisi zaidi kwa vikundi kwa madai
kuwa wanachama wamekuwa wakidhaminiwa na vikundi vyao, ambavyo ikiwa
mwanachama
huyo atakimbia basi kikundi hicho kitabeba mzigo wa
kumlipia.
Alitaja changamoto
kubwa inayowakabili hasa kwa wajasiriamali
wa mijini kuwa ni kutorejesha mikopo yao, jambo ambalo linasababisha
usumbufu
kwa SIDO na kuwafanya wengine wasikopeshwe fedha hizo.
Hata
hivyo alisema
kuwa mbali na mikopo hiyo, SIDO imekuwa
ikitoa mafunzo ya biashara kwa wajasiriamali, ili iwe rahisi kwao
kufanya
biashara kwa utaalam na kuweza kukuza biashara zao.
“Pamoja na mikopo
tumekuwa tukitoa mafunzo kwa wajasiriamali
wetu na kuwawezesha kushiriki kwenye maonyesho mbalimbali ndani na nje
ya nchi,
ili kutanua uelewa wa biashara zaidi,”alisema Mahinya.
Hata
hivyo aliwataka
vijana kuwa mstari wa mbele katika
kufanya kazi na SIDO ili waweze kuondokana na ugumu wa maisha ambao
umekuwa
ukiwakabili kwa kuamua kuwa wajasiriamali.
Alisema ikiwa vijana
watajikita kwenye ubunifu wa biashara,
itakuwa rahisi kuaminiwa na SIDO na hatimaye kupatiwa mikopo midogo
midogo
inayoweza kuwafikisha kwenye hatua ya kukopesheka na taasisi
nyingine.
0 comments:
Post a Comment