Msanii
wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flava, Shilole na wacheza show wake,
wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka msanii mwenzao wa Bongo Flava, Mez
B, mzaliwa wa Dodoma, wakati wa bonanza lililoandaliwa na Mfuko wa
Pensheni wa PSPF, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Februari 20,
2015. Bonanza hilo lilipambwa na michezo mbalimbali kama vile, soka,
netibole, voliboli na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa
na balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto wa Mjomba band. Wasanii wengine ni
pamoja na Chege na Temba na Mr. Blue. Mez B, ni mzaliwa wa mkoa wa
Dodoma, ambaye alifariki leo saa tano kwenye hospitali ya mkoa wa
Dodoma, alikokuwa akipatiwa matibabu. Anatarajiwa kuzikwa Jumatatu ijayo
Februari 23.
Chege(kulia) na Temba
Wanachuo na watu wengine wakipagawishwa na muziki uliokuwa ukiungurumishwa kwenye bonanza hilo
Mkuu
wa wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (wapili kulia) akiwa na Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, wakwanza kulia, wakati akitoa nasaha kwa
timu mbili za soka kutoka vyuo vikuu mkoani Dodoma
Maafisa wa juu wa PSPF, wakipasha misuli. Hata hivyo hawakuingian uwanjani kusakata kabumbu kutokana na muda kuwa mchache
Mchezaji wa timu ya Nertiboli ya chuo cha fedha CBE mkoani Dodoma, akiruka juu kumzuia mchezaji mwenzake kutoka UDOM.
0 comments:
Post a Comment