Nafasi Ya Matangazo

February 21, 2015


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah (kulia) na Rais wa Skauti Tanzania, Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia kwa Makamu) wakisimama kupokea maandamano ya Vijana wa Skauti, yalipokuwa yakiingia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell, leo Feb 21, 2015.
 Vijana wa Skauti wakipita mbele ya jukwaa kuu kwa maandamano wakati wa sherehe hizo za maadhimisho hayo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha Nishani ya Juu, Skauti Barnaba Abel, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Feb 21, 2015. Kulia ni Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania,  Abdulkarim Shah na (kulia kwa Makamu) ni Rais wa Skauti Tanzania, Dkt. Shukuru Kawambwa.
  Vijana wa Skauti wakipita mbele ya jukwaa kuu kwa maandamano wakati wa sherehe hizo za maadhimisho hayo.
 Vijana wakionesha michezo mbalimbali ya ukakamavu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Skauti baada ya sherehe hizo.
Posted by MROKI On Saturday, February 21, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo