Benki ya Dunia (WB) imeridhishwa na matokeo ya awali ya mradi wa
kuwasaidia wachimbaji wadogo awamu ya Kwanza na maboresho ya Mfumo wa
utoaji na usimamizi wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online
Mining- Cadastre) inayotekelezwa kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu
wa Rasilimali Madini Nchini (SMMRP) unaopata fedha kutoka Mkopo wa Benki
ya Dunia na HAZINA.
Kauli hiyo inafuatia kikao kilichojadili utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na SMMRP kilichofanyika hivi karibuni baina ya Idara ya Madini katika Wizara ya Nishati na Madini na Wawakilishi wa benki hiyo kilichojadili utekelezaji wa miradi hiyo, kuangalia namna bora ya kuendeleza utekelezaji wa Awamu ya Pili ikiwemo mikakati ya kuimarisha sekta ya Madini.
Akizungumza katika kikao hicho, Afisa Mwandamizi, Idara ya Nishati Endelevu, Mafuta, na Gesi ya Benki ya Dunia, Mamadou Barry alisema kuwa, Benki hiyo imeona na inatambua dhamira ya Serikali katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kutokana na utekelezaji ambao umefanywa katika awamu ya kwanza ya mradi huo.
0 comments:
Post a Comment