Na Father Kidevu Blog
Mkurugenzi wa
masuala ya sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,
Rugonzibwa Mujunangoma na Mhandisi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Theophil Bwakea wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kupokea Sh milioni 485
ambazo ni sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Washitakiwa
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka na
Wakili Leonard Swai kutoka Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Bwakea anadaiwa kupokea rushwa ya Sh milioni
161,700,000 kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya VIP Engineering and
Marketing ambaye alikuwa Mkurugenzi wa
kampuni ya IPTL James Rugemalira.
Anadaiwa
Februari 12, 2014 katika jengo la benki ya Mkombozi Ilala Dar es salaam, alipokea fedha kupitia akaunti namba
00410102643901 akiwa kama mjumbe aliyeandaa sera kuruhusu sekta binafsi
kuzalisha na kuiuzia umeme Tanesco.
Mbele ya Hakimu
Mkazi Emilius Mchauru, Mujunangoma anadaiwa kupokea Sh milioni 323,400,000,
baada ya kushughulikia masuala ya kampuni ya IPTL kama mfilisi jambo ambalo
linahusiana na kazi yake.
Anadaiwa kupokea fedha hizo
Februari 5, 2014, kupitia akaunti namba 00120102602001 kutoka kwa Rugemalira
ambazo ni sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Washitakiwa walikana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana baada ya
kutimiza masharti, Kesi hizo zitatajwa Januari 29 mwaka huu kwaajili ya
washitakiwa kusomewa maelezo ya awali lakini Januri 16 Mujunangoma atafika mahakamani
kukamilisha taratibu za dhamana.
0 comments:
Post a Comment