Meneja Mauzo wa AAR Insurance Bibi Tabia Massudi akiwaelezea wajasiriamali kuhusiana na Bima ya afya ya AAR kwenye mkutano wao na Wajasiriamali.
Mkurugenzi wa Bank ya Convenant,Bibi Sabetha Mwambenja akiwaelezea wajasiriamali kuhusu mikopo ya Bima ya Afya kwenye Mkutano ulofanyika jijini Dar es Salaam.
Wajasiriamali wakisikiliza maelezo wakati wa mkutano kati yao,Convenant Bank na kampuni ya Bima ya AAR jijini Dar es Salaam leo.
***********
Benki
ya wanawake ijulikanayo kama Convenant Bank pamoja na Kampuni ya bima
ya AAR washirikiana katika kuanzisha akaunti ya bima ya matibabu kwa
wajasiriamali walioko nchini .
Mkutano
kati ya Convenant Bank, AAR Insurance na wajasiriamali ulifanyika
mwishoni mwa wiki ilopita,uliohusika na kuwaelewesha wajasiriamali
kuhusu akaunti hiyo na umuhimu wa bima ya afya kwenye maisha yao ya kila
siku.
Akiongea
na wajasiriamali Mkurugenzi wa Convenant Bank Bibi Sabeth Mwambenja
alisema,“Akaunti hii ya Bima ni maalumu kwa watanzania wote wanaoohitaji
kupata bima ya matibabu kutoka AAR,akaunti hii inamuwezesha mmiliki
kupata bima ya matibabu na familia yake kwa mwaka mzima kwa shilling
1,000 kwa siku ambayo ni sawa na laki 360,000/= kwa mwaka”
“Benki
hii iliwafikria zaidi wajasiriamali na kuona AAR ni kampuni kubwa na
uhakika ya afya,lakini tuliona tuombe punguzo kubwa ambalo ni sawa na
nusu bei ya gharama ya bima ya afya ya kampuni hii,kwa kua tunatarajia
kupata kinamama 120,000 kutumia bima hii”. Alimalizia kusema Bibi
Mwambenja.
Pia
AAR ilipata nafasi ya kuwashukuru benki ya Convenant pamoja na
wajasiriamali wote walofika hapo na kuwapa elimu kuhusiana na bima ya
Afya.
Akiongea na wajasiriamali Meneja mauzo, Bibi Tabia Massudi alisema,“Ni
furaha kuwa wamoja katika kutoa mchango mkubwa katika kuwasaidia
wajasiriamali,ndio maana hatukusita kukubaliana na suala hili,kwasababu
tunajua umuhimu wa afya kwa binadamu na kwa wajasiriamali kama nyie,
karibuni sana mpate bima iliyo bora”.
0 comments:
Post a Comment