Nafasi Ya Matangazo

January 01, 2015

  Hii ilikuwa ni picha ya pamoja ya wasanii na mashabiki waliojitokeza kuunga mkono tamasha hilo la bure ambalo lina lengo la kuhamasisha vijana kushiriki katika maamuzi yenye mustakabali wa nchi.
WASANII wa muziki wa kizazi kipya, jana walitoa burudani ya aina yake pamoja na elimu kwa vijana juu ya ushiriki wao katika masuala ya nchi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Wakiongowa na  Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ pamoja na Niki wa Pili, wasanii aidi ya 10 waliwapagawisha mamia ya mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja hivyo kupata burudani na elimu hiyo.
Akizungumza kabla ya kuimba nyimbo zake kali,Mwana FA akitumia tamasha hilo lililopewa jina la ‘Tuonane Januari’, aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuchagua viongozi wanaowataka.
“Vijana wenzangu.., tusisubili watu wengine watufanyie maamuzi.., ni sisi wenyewe tunatakiwa kuamua tunachokitaka, tushiriki kwenye masuala nyeti ya nhi.., kuna uchaguzi mkuu unakuja, vijana tuwe mstari wa mbele na tuchague viongozi tunaowataka,” alisema Mwana FA.
Mara baada ya kusema hayo, alianza kuimba nyimbo zake zinabamba kwa sasa ukiwemo, mfalme ambao uliwapagawaisha mashabiki wengi viwanjani hapo.
Mbali nma Mwana FA, pia Niki wa pili alipata mapoekzi makubwa viwanani hapo kwa nyimbo zake kali huku pia akisisitiza vijana kuchakua maamuzi sasa ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Wanamuziki wengine waliokonga nyoyo za mashabiki wao ni pamoja na Shilole, Fid Q, Ditto, Linah, Navy and kenzo, Dogo Janja, Madee, Chegge, Temba, mwasiti na Stamina, ambao nyimbo zao ziliwafanya mashabiki waliojitokeza kuimba nao sambamba.
Tamasha hilo pia lilifanyika katika mikoa ya Njombe na Morogoro ambapo linalengo la kutoa elimu kwa vijana juu ya kuwa karibu na kushiriki matukio muhimu ya nchi hususani uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika Oktoba mwaka huu.
PICHANI jUU:  Mkali wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA akitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya sabasaba jana jioni mjini Morogoro. 
 Mtayarishaji nguli wa muziki wa kizazi kipya, Paul Mathyesse `P Funk' akichana mistari na msanii Fid Q katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar jana.
 Baadhi ya wakazi wa Temeke waliojitokeza kwenye onesho hilo la wazi lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar hapo jana.
Wasanii Chegge na Temba kutoka TMK Wanaume Family wakitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga
 Mkali mwingine wa kughani mitindo huru, Godzilla akitumbuiza jana jioni katika viwanja vya Mwembe Yanga,Temeke jijini Dar,kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika hapo jana.
Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
 Wasanii Aika, na Nahreel wanaounda kundi la Navy & Kenzo wakitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYang,Temeke jijini Dar.
Baadhi ya wadau wakirekodi tukio muhimu
 Pichani Msanii Mwasiti akiimba wimbo wake wa serebuka mbele ya mashabiki wake huku shangwe za mayowe na vifijo zikiwa zimetawala uwanjani hapo  jana.
Wasanii Madee na Dogo Janja ( hayupo pichani) wakitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar.
Posted by MROKI On Thursday, January 01, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo