Meneja Idara ya
Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi. Kissa Mwamwitwa (aliyesimama),
akimtambulisha Mgeni Rasmi, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Samson
Tarimo (katikati) aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TFDA (Bw. Hiiti B. Sillo),
katika ufunguzi wa Warsha husika kwa
washiriki (hawapo pichani). Kulia ni Mshauri wa Masuala ya Afya na Mipango
(Public Health Logistics Advisor) wa Shirika
Lisilo la Kiserikali la Kimataifa la JSI Bi. Elika Mmari.
**************
Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Kimataifa la John
Snow Inc (JSI) wameandaa warsha ya siku
mbili kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa Uhamasishaji, Uelimishaji na Ufuatiliaji wa
karibu wa utoaji taarifa za madhara yanayohisiwa kusababishwa na dawa katika mikoa minne (4) ya majaribio ya Dodoma,
Singida, Tabora na Kigoma.
Warsha hiyo imehusisha wataalam wa sekta ya afya zaidi ya 30 kutoka
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, TFDA, JSI,
Christian Social Services Commission
(CSSC), Elizabeth Glaser Pediatric
AIDS Foundation (EGPAF) na wawakilishi kutoka mikoa saba ya Tabora, Dodoma,
Singida, Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza na Dar es Salaam ambao kwa pamoja
walijadili mada zilizowasilishwa kuhusu uzoefu uliopatikana kutoka katika mikoa
minne iliyofanyiwa majaribio, changamoto zake na jinsi ya kukabiliana nazo ili
kuleta ufanisi wa kazi hiyo katika mikoa yote kwa lengo la kulinda afya ya
jamii.
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa warsha hiyo alikuwa ni Kaimu Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Samson Tarimo ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa
TFDA Bw. Hiiti B. Sillo.
Aidha. wilaya za Kibondo, Urambo, Kondoa na Iramba zilipata tuzo za
vyeti kwa kukusanya taarifa nyingi kuliko wilaya nyingine zilizokuwa katika
mradi wa majaribio hayo. Vyeti hivyo vilitolewa na Mgeni Rasmi ambaye
aliwakilisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika ufungaji wa warsha
hiyo, Bw. Dikson S. Kejo.
Baadhi
ya washiriki katika Warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi
kutoka kwa Mgeni Rasmi (hayupo pichani).
Afisa Programu na Utawala wa
Usambazaji kutoka Shirika Lisilo la Kiserikali la Kimataifa la Elizabeth Glaser
Pediatric AIDS Foundation (EGPAF), Bw. Brendan Lyimo (aliyesimama) akiwasilisha
mojawapo ya mada kwa washiriki.
Mshauri wa Masuala ya Afya na
Mipango (Public Health Logistics Advisor) wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Kimataifa la JSI Bi.
Elika Mmari akionesha washiriki (hawapo pichani), mojawapo ya vielelezo
vinavyotumika katika kuelimisha na kuhamasisha ukusanyaji wa taarifa
zinazohisiwa kusababishwa na madhara yatokanayo na matumizi ya dawa.
Mgeni Rasmi katika sherehe za
kufunga warsha husika, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. . Dikson
S. Kejo (aliyesimama nyuma kulia) akimkabidhi mmojawapo wa washiriki, tuzo ya cheti kwa kufanya vizuri katika
ukusanyaji wa taarifa zinazohisiwa kusababishwa na madhara yatokanayo na
matumizi ya dawa.
Washiriki wakiwa katika picha
ya pamoja wakati wa ufunguzi wa Warsha husika. Waliokaa, ni Mgeni Rasmi Kaimu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Samson Tarimo (katikati), Mwakilishi
kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. Dikson S. Kejo (wa pili kutoka
kulia), Mshauri wa Masuala ya Afya na Mipango (Public Health Logistics Advisor)
wa Shirika Lisilo la Kiserikali la
Kimataifa la JSI Bi. Elika Mmari (kulia) na Meneja Idara ya Majaribio na
Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi. Kissa Mwamwitwa (wa pili kushoto).
0 comments:
Post a Comment