Nafasi Ya Matangazo

January 03, 2015

SAM_0611
Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Felix Ntibenda wa pili kulia akikabidhi hundi  ya shilingi milioni 17na laki tano kwa wajasiliamali wa MT meru curios &crafts market wanaojishughulisha na uzaji wa bidhaa za vijago jijini walizo kopa kwa ajili ya kufanya biashara kabla wa soko lya kunguliwa na soko hilo mapema mwezi uliopita
SAM_0617Meneja wa  taasisi hiyo Baraka Jekonea akiongea na vyombo vya habari
SAM_0613
Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Felix Ntibenda akiongea katika halfa hiyo
SAM_0614
Muonekano wa soko jipya
Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Felix Ntibenda ameipongeza taasisi inayotoa huduma za kifedha (FINCA)kwa kuwafutia  zaidi ya milioni 30 wanachama 35  wajasiliamali wa MT meru curios &crafts market wanaojishughulisha na uzaji wa bidhaa za vinyago hela walizo kopa kwa ajili ya kufanya biashara kabla ya soko loa kunguliwa  mapema mwezi uliopita.

Ntibenda alisema  hayo jana wakati akikabidhi hundi  ya shilingi milioni 17na laki tano kwa wajasiliamali hao  mbele ya waandishi wa habari iliyofanyika eneeo la soko hilo lililoko wilaya ya arusha mkoa wa arusha.

Kwa upande wa meneja  taasisi hiyo Baraka Jekonea alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuendeleza ujenzi wa  soko hilo I benki hiyo in warudi katika hali yao ya zamahi ya biashara .

“Sisikama Taasisi ya Kifedha Finca tumeamua kuwasaidia ili tuweze kuwanusuru wahanga hawa kwa janga walilolipata tunaimani kwamba watarejea katika hali yao ya zamani kwani tangu wakumbane na changamoto hiyo maisha yao yamekuwa magumu sana”alisema Jekonea

Pia alitoa wito kwa wafanyabiashara ambao hawajajiunga na taasisi hiyo kufanya hivyo kwa kuwa benki hiyo inajali wajasiriamali na kuwataka kujiunga na taasisi ya mikopo ili kuweza kupata mikopo ya nafuu.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa soko hilo Hamis Juma alishukuru taasisi kwani pesa hiyo itawasaidia sana sana katika kujikwamua na kurejesha hali yao ya awali katika biashara yao.

Hata hivyo kabla ya msaada   huo walijichangisha kiasi cha shilingili laki nane kwa kila muhanga nakufanikiwa kukusanya shilingi milioni mia mbili iliyowasaidi kuanza ujenzi wa soko hilo.

Aidha mwenyekiti huyo ameomba taasisi nyingine ili kuweza kuwasaidia kuwapatia mitaji ili kuweza kuanza upya tena biahsra hiyo ya uuzaji wa vinyago.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Posted by MROKI On Saturday, January 03, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo