Hatua ya robo fainali ya michuano ya
Kombe la Taifa kwa Wanawake inachezwa kesho (Januari 26 mwaka huu) na Januari
27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam
kwa mechi mbili kila siku.
Mechi ya kwanza ya robo fainali ya
michuano hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Televisheni itaanza saa 9
alasiri kwa kuzikutanisha Mwanza na Kigoma. Robo fainali ya pili ambayo ni kati
ya Tanga na Pwani itaanza saa 11 kamili jioni.
Ilala na Iringa watacheza robo fainali
ya tatu Januari 27 mwaka huu kuanzia saa 9 kamili alasiri, na kufuatiwa na robo
fainali ya mwisho saa 11 kamili jioni itakayozikutanisha Temeke na Mbeya.
Nusu fainali za michuano hiyo
inayodhaminiwa na kampuni ya Proin zitachezwa Januari 29 mwaka huu wakati
Fainali itachezwa Februari Mosi mwaka huu kuanzia saa 10.15 jioni ambapo
itatanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu (play off).
Timu zote zilizoingia hatua hiyo ya nane
bora ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini zimefikia hosteli
ya Msimbazi.
Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo
utafanyika kesho (Januari 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF
zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
0 comments:
Post a Comment