Nafasi Ya Matangazo

January 05, 2015

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba wakati alipowasili jimboni humo katika wilaya ya Lushoto. akiwa katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Mponde na kuwataarifu wananchi na wakulima wa Chai kuhusu maagizo ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kukirejesha kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi , Awali kiwanda hicho kilikuwa kinamilikiwa na Mwekezaji Yusuf Mulla na kilifungwa kutokana na mgogoro wa wakulima wa Chai na mwekezaji huyo . Rais Jakaya Kikwete amechukua uamuzi huo baada ya katibu Mkuu wa CCM Ndugu Andulrahman Kinana kusikiliza kero hiyo ya wananchi wakati alipofanya ziara ya mkoa wa Tanga na kuahidi kufuatilia ili kuhakikisha suluhisho la kudumu linapatikana na wakulima hao wanapata haki yao. Mgogoro huo umedumu kwa muda wa miaka kumi na kiwanda hicho kimefungwa kwa muda wa miezi ishirini kabla ya Rais Jakaya Kikwete kufikia uamuzi wa kukirejesha kwa wananchi. 2Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukiwasili katika eneo la mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Mponde katika jimbo la Bumbuli wilayani 5Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye eneo la mkutano wa hadhara. 6 7Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. Majid Hemed Mwanga akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kijiji cha Mponde mkoani Tanga. 8Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mh. Mrisho Gambo akisalimia wananchi katika mkutano huo. 9 Mmoja wa wananchi kijiji cha Mpond akipiga makofi huku akiwa amevaa sanamu 10Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Magalula Said Magalula akisalimiana na wananchi na kujitambulisha kwao kama mkuu wa mkoa huo. 11Mbunge wa jimbo la Lushoto Henry Shekifu akiwahutubia wanamponde. 12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa na wakulima wa Chai Mponde wakati alipofika kijijini hapo ili kuwataarifu juu ya rais Jakaya Kikwete kuamuru Kiwanda cha Chai cha Mponde kurejeshwa kwa wananchi. 13 17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiongea na wananchi katika mkutano huo wa hadhara.
Posted by MROKI On Monday, January 05, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo