Doris Mollel akisema Maneno machache wakati akikabidi mashine mbili za watoto kupumulia zenye thamani ya Tsh millioni 1.2 kwa hospitali ya mkoa wa Singida kwa ushirikiano na Manifester brand.
*******
Na mwandishi wetu, Singida.
Katika kuianza safari yake ya huduma za jamii kwa mwaka
2015, Redds Miss central zone2014-2015 Doris Mollel ametoa msaada wa mashine 2 za
kupumulia kwenye hospitali ya mkoawa Singida zenye thamani ya Tsh 1,200,000/=. Mashine hizo
huwasaidia watoto waliozaliwakabla ya muda wa kawaida (Pre-mature babies) katika mfumo
wao wa upumuaji ambao huhitajimsaada wa juu zaidi mara tu wanapozaliwa.
Doris ambaye pia ni mshindi wa tatu wa Redds Miss
Tanzania 2014 ni mwanaharakati wadhana ya Urembo wenye Malengo endelevu kwa jamii ‘Beauty
with a Purpose’. Amefanyakazi kubwa kwenye sekta ya elimu akijikita zaidi kwenye
kuchangia Vitabu kwa shule za msingina sasa, akiwa ni mmoja ya watu ambao walizaliwa kabla ya
muda wa kawaida ameamuakupanua wigo wake wa huduma za jamii kuleta mwamko na
kusaidia kuokoa maisha ya watotohawa.
Akiongea kwenye hafla ya kukabidhi mashine hizo
iliyofanyika hospitalini hapo, Mollel alisema.“Kiwango cha vifo kwa watoto wanaozaliwa kabla ya kukomaa
ni karibu 30% vikichangiwa kwakiasi kikubwa na ukosefu wa vifaa vya kutosha kusaidia
mifumo yao ya upumuaji mara tuwanapozaliwa. Nikiwa moja ya watoto hao ambaye
nilibahatika kupata msaada na huduma yakutosha nilipozaliwa, Ninaelewa ni jinsi gani matunzo
haya ya awali yalivyo muhimu kwenyekuokoa maisha ya watoto hawa na ninajikita kuwasaidia”
Bw. Albert Mbepera, Mkurungezi wa Albert Manifester
Photojournalism; kitengo ndani ya Manifester brand kilichojikita kwenye masuala ya jamii
alisema ‘huduma kwa jamii ni eneo muhimu sana kwetu. Tunafurahi kujitolea kufanya kazi na
Doris katika maswala ya kusaidia jamii na tunaamini kuwa ushirikiano huu utasaidia
kukusanya na kuonyesha matatizo ya wahitaji ili kuongeza uelewa na msukumo wa misaada kutoka kwa
sekta binafsi na wanajamii kwa ujumla’
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni mkuu wa wilaya
ya Singida Bi Queen Mlozi na ilihudhuriwa na Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa
Singida Bw. Daniel Tarimo, Daktari bingwa wa watoto wa Hospitali ya Singida, Muandaaji wa
Redds Miss Singida 2014 Bora Lemmy na washindi wengine wa Redds Miss central Zone Linda
Bureta, blath Chambia, Suzy Wahere.
Doris akikabidhi mashine 2 za msaada wa
watoto kupumulia zenye thamani ya Tsh milioni 1.2 kwa mganga mfawidhi wa
hospitali ya mkoa wa Singida Dk. Daniel Tarimo, msaada kwa ushirikiano na
Manifester brand. Mgeni rasmi kwenye hafla hii alikua ni mkuu wa wilaya ya
Singida Bi. Queen Mlozi (hayupo pichani).
Doris
katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi, Mganga
mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dk. Daniel Tarimo, Muandaaji wa Miss
Singida Bi. Bora Lemmy na warembo wengine wa Redds miss Central Zone.
Doris kwenye
picha ya pamoja na warembo wenzake wa central zone walioenda kumuunga mkono.
Linda Bureta, Blath Chambia na Suzy Wahere.
Doris akiangalia mmoja wa watoto
Mtoto aliyezaliwa kabla ya muda wa kawaida akiwa kwenye
mrija wa kumsadia kupumua uliounganishwa na mashine kama ambazo zimekabidhiwa
na Doris.
Alipata
nafasi ya kuwasimulia baadhi ya kina mama waliojifungua watoto njiti kuhusu historia
yake na kuwapa moyo kwamba hata watoto wao pia watakua na kufanikiwa kufika
popote pamoja na kuzaliwa njiti.
0 comments:
Post a Comment