Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (M-NEC) Ndugu Sixtus Mapunda amesema kuwa
Chadema wamepanga njama haramu za kuvuruga uchaguzi wa Serikali za
mitaa kwa kuwaandaa vijana wa kufanya vurugu na kuwazuia akina mama
na wazee wasiende katika maeneo ya kupigia kura.
Mapunda
ameyasema hayo leo majira ya saa tano na nusu asubuhi wakati
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwanzugi Kata ya Igunga ,
mkoani Tabora ambako yupo katika ziara ya Kikazi ya siku kumi na nne
katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera.
“..tumepata
taarifa za kuaminika kuwa Chadema wameandaa vijana na kuwaandalia
viroba na bangi ili waweze kufanya vurugu siku ya uchaguzi na
kuwazuia wananchi kwenda kupiga kura katika vituo
vilivyoandaliwa.,tunawataka waache mpango huo mara moja kwani
vyombo vya dola viko macho na vitawachukulia hatua wote watakaofanya
hujuma hizo..”
alisema
Mapunda katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mwanzugi stendi
na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa kijiji cha Mwanzugi.
Pia,
Mapunda amewataka wananchi kuwachagua Viongozi wanaotokana na Chama
Cha Mapinduzi kwani ni waaminifu, wakweli na wenye anuani kamili kwa
maana ya kuwa wanazo ofisi zinazotambulika katika kila kijiji na Kata
ambako wananchi wanaweza kupeleka malalamiko yao na kusikilizwa
tofauti na vyama vingine ambavyo havina ofisi wala anuani ya Kudumu.
Mapunda
ameendelea na mikutano yake ya hadhara katika Mkoa wa Tabora ambako
anatarajia kuzungumza na wananchi wa wilaya za Kaliua, Urambo na
Nzega.
0 comments:
Post a Comment