Nafasi Ya Matangazo

November 26, 2014

 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu Siku ya Takwimu Afrika itakayo adhimishwa Dar es Salaam kesho. Kulia ni Mtakwimu Mkuu, Adella Ndesengia. 
 " Nilazima picha hii niipate hata iweje' kama anaongea Ofisa Habari wa NBS, Veronika Kazimoto wakati akichukua taarifa hiyo kwa njia ya picha- kweli mama yupo kazini -chezea kazi wewe.
 wanahabari wakichukua tukio hilo.
 Mkrugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa yaTakwimu imeitaka jamii  kutoa ushirikiano wakati wa ukusanyaji wa taarifa za matumizi,kwamba husaidia kuandaa sera na kupanga mipango ya maendeleo nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam  na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo wakati akitoa taarifa ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika kesho.

"Maadhimisho ya siku ya siku ya takwimu Afrika hufanyika kila ifikapo Novemba 18 kila mwaka, kwa Tanzania tumechelewa kwa sababu ya utekelezwaji wa majukumu mengine ya kiserikali, hivyo maadhimisho hayo yanafanyika leo," alisema Kwesigabo.

Kwesigabo alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa tasinia ya takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.


Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa  kuwa ni Waziri wa Fedha kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Yosuf Mzee na kwamba wadau wengine watakaoshiriki ni  wizara, Idara na Taasisi za Serikali, wadau wa maendeleo,vyuo vya elimu ya juu,wadau wengine wa takwimu nchini.OFISI ya Taifa yaTakwimu imeitaka jamii  kutoa ushirikiano wakati wa ukusanyaji wa taarifa za matumizi,kwamba husaidia kuandaa sera na kupanga mipango ya maendeleo nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam  na Mkurugezi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii,Ephaim Kwesigabo wakati akitoa tarifa ya maathimisho ya siku ya takwimu Afrika.

"Maadhimisho ya siku ya siku ya takwimu Afrika hufanyika kila ifikapo novemba 18 kila mwaka,kwa Tanzania tumechelewa kwa sababu ya utekelezwaji wa majukumu mwengine ya kiserikali,hivyo maadhimisho hayo yanafanyika leo,"alisema.

Kwesigambo alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa tasinia ya takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.

Mgeni rasmi anaetarajiwa katika maadhimisho hayo ni waziri wa fedha kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Yosuf Mzee na kwamba wadau wengine watakaoshiriki ni  wizara,Idara na Taasisi za Serikali,wadau wa maendeleo,vyuo vya elimu ya juu,wadau wengine wa takwimu nchini. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)


Posted by MROKI On Wednesday, November 26, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo